• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RC Chalamila Aaagiza Majina 891 Yaliyohakikiwa Kupatiwa Vizimba Kariakoo Yaondolewe Kwenye Mfumo

Posted on: July 12th, 2024

 

-Ataka mchakato wa kuwapata wafanyabiashara kuanza upya na ufanyike kwa uwazi na majina yatahuishwa kwa pamoja kwenye mfumo baada ya kupitiwa na Taasisi kadhaa kujiridhisha

-Aagiza TAKUKURU Mkoa kufutilia kwa karibu Shirika la masoko Kariakoo

-Atoa wiki mbili Bodi na Mtendaji Mkuu wa Shirika la masoko Kariakoo kujitathimini

-Amtaka Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kupitia taarifa za watumishi wa shirikia hilo kujua wamekaa kituo hicho kwa muda gani.

-Aagiza wafanyabiashara waliotumia ujanja kujipatia kibanda zaidi ya kimoja wachukuliwe hatua.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 12, 2024 kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya kikao na wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la machinga na watumishi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo.

RC chalamila akiongea na wafanyabishara katika ukumbi wa ofisi yake Ilala Boma alipata wasaa wa kuwasikiliza kwa kina malalamiko na kuwahakikishia Serikali ya Mkoa iko makini sana mfanyabiashara ambaye atakuwa na janja janja ya kujipatia kibanda zaidi ya kimoja hatua kali zitachukuliwa dhidi yake “Kamwe siasa kariakoo hazikubaliki nitasimama imara” Alisema Chalamila.

Aidha RC Chalamila baada ya kuongea na mamia ya wafanyabiasha hao alifanya kikao kingine na watumishi wa shirika la Masoko Kariakoo ambapo ameagiza kushushwa kwa majina 891 kwenye mfumo ili kufanyika upya kwa uhakiki tena kwa uwazi ili kusiwe na malalamiko ya wafanyabiashara.

Sanjari na hilo RC Chalamila ameagiza TAKUKURU Mkoa kufuatilia kwa karibu Shirika la Masoko Kariakoo na kuitaka Bodi ya Shirika hilo pamoja na mtendaji mkuu ndani ya wiki mbili kuanzia leo kujitathimini juu ya malalamiko ya vitendo vya Rushwa yanayotolewa na wafanyabiashara kwa Shirika hilo.

Vilevile amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila ndani ya wiki moja kupitia taarifa za watumishi wa shirika la masoko Kariakoo kujua wamaekaa katika kituo hicho muda gani pia ufanisi katika utendaji wao wa kazi aidha ameelekeza wakati wa uhakiki mfanyabiashara atakayebainika kujipatia kwa ujanja kibanda zaidi ya kimoja achukuliwe hatua stahiki

Mwisho RC Chalamila amesema katika Soko la Kariakoo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kukarabati na kujenga Soko jipya hivyo uendeshaji wake lazima uwe wa kidigitali pia kila mmoja atambue soko la Kariakoo ni la Kimataifa hivyo hata muonekano wake na mazingira yake lazima yawe nadhifu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa