• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Rasilimali za Bahari Zinamchango Mkubwa katika Kukuza Uchumi

Posted on: September 30th, 2024

 

Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba Nguvila amesema Sekta ya Uvuvi ikisimamiwa vyema kupitia rasilimali za Bahari ya Hindi ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi, sekta hiyo itaweza kuimarisha pato la taifa kupitia mnyororo wa thamani.

Dkt. Nguvila amesema hayo leo septemba 19, 2024 katika ukumbi wa Mikutano Anartoglo - Ilala wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe Albert Chalamila, kwenye ufunguzi wa mkutano uliohusisha kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na viongozi wa wilaya za Ilala, Kigamboni, Temeke na Kinondoni zenye maeneo yenye bahari.

Dkt Toba Nguvila amesema kuwa mnyoyoro huo wa thamani unaohusisha wadau wa Sekta ya Uvuvi wakiwemo wavuvi wenyewe, kwenye masoko na wachakataji wa mazao ya uvuvi utakuwa na tija kwa kuhakikisha ulinzi wa rasilimali za uvuvi unazingatiwa ili kupata fedha nyingi kupitia biashara ya mazao hayoambapo amesema Samaki wanaovuliwa wakiwa wadogo kwenye soko hawaingii hivyo hauwezi kupata hesabu yao kwenye pato la taifa, hii inamaanisha ni uvuvi haramu lakini tukilinda rasimali za uvuvi vyema watavuliwa samaki wanaohitajika na pato la taifa litakuwa kubwa hivyo kukuza uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja

Aidha, ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufanya tafiti zaidi ili vizimba vya kufugia samaki viweze kutumika pia katika upande wa bahari kuu kwa kuwa yapo maeneo ambayo yanaweza kufaa kwa ajili ya uwekaji wa vizimba.

Sambamba na hilo amesema ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba kwa bahari kuu utasaidia kuwawezesha wadau wa Sekta ya Uvuvi kupatiwa mikopo na kufuga samaki kwa tija na kutoa fursa ya kupatiwa elimu ya ufugaji huo na kuondokana na dhana ya uvuvi haramu.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayesimamia Sekta ya Uvuvi Dkt Edwin Mhede, amesema wizara imepewa mamlaka ya kuhakikisha kunakuwa na uvuvi endelevu kama moja ya mbinu ya kulinda rasilimali za uvuvi hazipotei na zinavuliwa kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo.

Dkt. Mhede amesema mkutano huo unalenga kukumbushana majukumu na umuhimu wa kuongeza ufanisi ili ulinzi wa rasilmali za uvuvi unaotakiwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uweze kutekelezwa na kwamba itaendelea kusimamia hilo.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uvuvi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohamed Sheikh amesema lengo la mikutano ya kukutana na kamati za ulinzi na usalama za mikoa ni kuwa na mikakakti mbalimbali ya kuhakikisha rasilimali za uvuvi katika maji yote ya asili zinalindwa ili kuwa na tija katika pato la taifa.

Ameongeza kuwa kumewekwa mikakati mbalimbali ya muda mrefu, mfupi na kati kwa kushirikisha wadau ili kuwa na makubaliano ya pamoja ya namna ya kulinda rasilimali za uvuvi na kuhakikisha rasilimali hizo zinazidi kuzaliana kwa wingi na kuongeza uhitaji katika masoko.

Nao baadhi ya washiriki wamesema mkutano huo umekuja muda muafaka katika kuelimishana na kuwa na mawazo ya pamoja ya kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinazidi kulindwa na kuwa na tija kwa taifa.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa