• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RAS NGUVILA : "MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA NA TAASISI ZA SERIKALI SHIRIKIANENI VEMA SIO KUTUNISHIANA MISULI"

Posted on: May 17th, 2024

 -Afungua na kufunga Kikao kazi Cha Robo Mwaka 

-Aelezea Umuhimu wa Kikao kazi Cha Robo Mwaka 

-Atoa Maagizo yafuatayo kwa MSM na Taasisi za Serikali Dsm 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt.Toba A. Nguvila amezitaka Taasisi za Serikali na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM) kushirikiana vema katika kutoa huduma kwa wananchi na sio kutunishiana misuli wao kwa wao Dkt. Nguvila ameyasema hayo Jana tarehe 17 Mei, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arnatoglo uliopo Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Kikao kazi Cha Robo Mwaka ambacho kilifanyika kwa Mara ya mwisho 2019 

RAS Nguvila ameongeza kuwa Uratibu na Usimamizi wa Kikao kazi hicho unafanywa na Sekretarieti ya Mkoa kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Tawala za Mikoa Sura namba 97 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2002 

Aidhaa, Katibu Tawala ameeleza kuwa Kikao kazi hicho ni muhimu kwa ajili ya kumuwezesha kupata taarifa za utekelezaji wa Miradi, Ukusanyaji wa mapato na utendaji kazi wa jumla wa Halmashauri na Taasisi za Umma zilizopo ndani ya Mkoa Dkt. Nguvila ameyataja maagizo mbalimbali yaliyotolewa na Mamlaka Kama vile:- -Matumizi ya Mifumo ya kielektroniki katika Ukusanyaji wa mapato, Watendaji wa Serikali kwenda "field" kusimamia miradi sio kukaa ofisini, Watendaji kutatua kero za wananchi, Kujibu Hoja za Ukaguzi kwa wakati, Kudhibiti matumizi ya fedha za umma, Wabadhirifu wa fedha za Umma kuchukuliwa hatua stahiki, Ulipaji wa Madeni ya watumishi, Kuboresha na Kupendezesha Mandhari ya Jiji la Dsm, Utekelezaji wa Mkakati wa Taifa dhidi ya Rushwa, Matumizi ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ikiwemo matumizi ya mfumo wa NEST na Utekelezaji wa Mfumo wa "Pepmis na Pipmis" 

Hata hivyo, RAS Nguvila ametoa maagizo yafuatayo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Serikali Kama ifuatavyo:- *-DAWASA*- kuona namna ya kuwarejeshea huduma wadaiwa sugu waliokatiwa maji miaka mitano au zaidi kwa kuweka mikataba mipya ya ulipaji kwa lengo la kupanua wigo wa kukusanya mapato *-TRA na MSM* - Elimu ya EFD itolewe na iwe endelevu *-TANESCO*- Wakandarasi wanaochelewesha miradi ya Maendeleo wachukuliwe hatua kwa mujibu wa mkataba ikiwemo kuvunja mkataba *-TARURA,TANROADS na MSM*- Malori yote yanayopaki barabarani yaondolewe Mara moja *-BONDE LA RUVU*- taratibu za kuchimba mchanga zifuatwe, Kodi ilipwe, Vibali visitoke ovyo ovyo, mifugo ikiingia ipigwe faini kwa mujibu wa Sheria na usimamizi wa uchimbaji wa visima *-NEMC*- Yatakiwa kushauri Mahali pa kupelekea maji machafu yanayotiririka kutoka viwandani *-MSM na Taasisi za Serikali* kuelezea kwa wananchi miradi ya kimkakati inayotekelezwa (inayofanywa) na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan *

Ikumbukwe kuwa Kikao kazi hicho kilikuwa Cha siku mbili yaani tarehe 16 -17 Mei, 2024 ambapo watendakazi hao walitumia Kikao hicho kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika maeneo yao*


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa