• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RAS Nguvila Afanya Ziara Usiku wa Manane Hospitali ya Mbagala Rangi Tatu

Posted on: September 7th, 2024

 

-Akuta huduma nzuri inatolewa hospitalini hapo

-Abaini wingi wa wagonjwa hospitalini hapo na uchache wa watumishi na kumuagiza Mkurugenzi na DMO kuongeza watumishi

-Aagiza RMO, DMO's  kutembelea Hospitalini ,Vituo vyao Afya na Zahati usiku na mchana kukagua huduma zinazotolewa huko

-Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una akiri kupokea maelekezo na kuahidi kuyasimamia ipasavyo

-Baadhi ya ndugu za wagonjwa waliokuwepo hapo wasema huduma hapo ni nzuri

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Toba A. Nguvila akiambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una amefanya ziara ya kushtukiza ya  usiku wa manane  tarehe 06 Septemba, 2024  katika Hospitali ya Wilaya ya Mbagala Rangi tatu na kukuta huduma nzuri inatolewa katika Hospitali hiyo

Dkt. Nguvila amebaini uwepo wa wagonjwa wengi wanaofika kuhudumiwa katika Hospitali hiyo na uchache wa watumishi wanaotoa huduma na kumuagiza  hapo hapo Mkurugenzi wa Temeke kupitia Idara ya Afya kuhakikisha wanaongeza watumishi katika Hospitali hiyo ili kupunguza msongamano wa wagonjwa sambamba na kupata huduma Bora kwa wakati

Hata hivyo RAS Nguvila amemuagiza RMO, DMO's  kutembelea katika Vituo mbalimbali vya Afya usiku na mchana ili kujionea huduma zinazotolewa huko na kuyafanyia kazi mara Moja mapungufu pindi wanapokutana nayo

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Mang'una amekiri kupokea maagizo yote yaliyotolewa na Katibu Tawala wa Mkoa na kuahidi kuyasimamia ipasavyo ili wananchi wa Temeke waendelee kupata huduma Bora za Afya, aidha amewaasa wananchi wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano yaliyopo pindi wanapopatwa na kadhia yoyote ili kadhia zao zipatiwe ufumbuzi wa haraka

Wakati huo huo baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliokuwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali hiyo wamepongeza huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo na kusema kuwa ni nzuri sana

#Chini ya Uongozi wa SSH tutoe huduma nzuri za Afya

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa