• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

RAS Madenge Afungua Mafunzo ya Kimkakati kwa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI Mkoa

Posted on: July 27th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge Akiongea wakati wa mafunzo hayo.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi Rehema Madenge leo Julai 27, 2023 amefungua mafunzo ya kimkakati kwa Kamati ya kudhibiti UKIMWI ngazi ya Mkoa.

Akiongea wakati wa mafunzo hayo amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza afua za mwitikio wa kitaifa dhidi ya VVU na UKIMWI kwa zaidi ya miongo mitatu (3) tangu kugundulika kwa ugonjwa huo.

Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa makini wakati wa mafunzo hayo.

Hata hivyo miongoni mwa majukumu ya msingi yanayo tekelezwa ni pamoja kuandaa mpango mkakati wa afua za VVU na UKIMWI pia kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa afua hiyo.

Kwa dhana hiyo Sekretarieti ya Mkoa inajukumu la kuratibu utekelezaji wa masuala ya UKIMWI katika mamlaka za Serikali za Mitaa vilevile Sekretarieti zimetakiwa kuwa na timu au Kamati za kudhibiti UKIMWI (Regional AIDS Team) ambayo ndio hii kupitia wote tuliojumuika hapa

Aidha Bi Rehema Madenge amesema lengo la kamati hii ni kuimarisha uratibu na usimamizi wa afua za VVU na UKIMWI katika Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili zifanye kazi zake za uratibu na usimamizi kwa ufanisi, hivyo kila aliyoko kwenye kamati hii anajukumu kubwa la kufanya kwa mstakabali wa ustawi wa jamii.

Sambamba na hilo mafunzo hayo yameweza kuainisha hali ya VVU na UKIMWI katika Mkoa, wajumbe wamepitishwa kujua mwongozo wa kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi, mfumo wa uratibu, mwongozo wa kuziwezesha Sekretarieti za Mikoa kuratibu utekelezaji wa masuala ya UKIMWI katika mamlaka za Serikali za mitaa na Maazimio ya hatua zinazofuata.

Mwisho wajumbe walipata wasaa wa kutoa maoni na michango yao kwa lengo la kufikia dhamira ya Serikali ya kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu yasiyoambukiza mahala pa kazi

Baadhi ya matukio katika picha wakati wa mafunzo hayo mapema leo.

Matangazo

  • MWENENDO WA BEI YA 02-06 FEBRUARI 2026 DSM February 10, 2026
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • MWENENDO WA BEI WIKI YA 1-5 DESEMBA 2025 December 01, 2025
  • MWENENDO WA BEI YA WIKI YA 26-30 JANUARI 2026 DSM February 09, 2026
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalimila Aendelea Kuchanja Mbuga Wilaya ya Kinondoni

    February 12, 2026
  • RC Chalamila Achukizwa na Kasi ndogo ya Utekelezaji wa Miradi ya BRT Kinondoni

    February 11, 2026
  • Uzinduzi wa Soko Jipya la Kariakoo

    February 08, 2026
  • RC Chalamila Ataka Walimu Kutafsiri Vema Maono ya Rais Samia

    February 06, 2026
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa