• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Rais Samia Amefanya Mambo Makubwa DSM

Posted on: November 4th, 2023

 

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Albert Chalamila amesema hayo leo Novemba 4, 2023 wakati wa mkutano maalum wa uwasilishaji wa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi Mahiri wa Dkt Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa Yombo (wa chuo kiku cha Dar es salaam)
RC Chalamila alisema chini ya uongozi mahiri wa raisi  Dkt Samia Suluhu Hassan wananchi wengi wamesikika na wamefikiwa kwa kuboreshewa na kutatuliwa kero na matatizo yao yaliyokuwa yanawasumbua ikiwemo maji, barabara, umeme, afya, usafiri wa mwendo kasi n.k
Aidha Mhe Chalamil aligusia suala la mshikamano, ushirikiano na amani ambayo ni tunu na rasilimali kwa maendeleo ya nchi wa uwepo wa vyombo vya dola imara ambapo kati ya asilia Mia moja basi asiliamia 95 vyombo hivyo vinafanya kazi nzuri iliyopelekea mpakaTanzania kuwa wenyeji wa mikutano mikubwa ya kimataifa.
Vilevile RC aligusia sekta nyingine mbalimbali zilivyoboreshwa ikiwemo elimu kwa kufuta ada ya kidato cha  tano na sita, kuboresha miundo mbinu ya shule kwa kujenga madarasa na nyumba za walimu, mikopo kwa elimu ya juu imeongezeka mpaka elf 10 kwa siku na kuongezeka kwa idadi ya wanufaika.
Pia RC Chalamila alimpongeza Mhe Raisi Dkt Samia maendeleo ya usafiri wa anga kwa kuboresha viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege kubwa yenye kubeba watu 180 na ndege nyingine ya mizigo zitakazosaidia usafirishaji wa bidhaa zetu hasa zile za kuharibika haraka ikiwemo mazao ya mashambani kwenda nje ya nchi, "Mpaka sasa tuna ndege 13 ambazo zinamilikiwa na shirika la ndege la Tanzania," alisema.
Wakati akijibu maswali kutoka kwa wananchi na waandishi RC Chalamila aligusia suala la bandari ambapo amefafanua uwekezaji uliofanywa ni mkubwa na utatuletea manufaa ni wajibu wetu kuendelea kumuunga mkono Mhe Raisi Dkt Samia.
Naye msemaji mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi alimshukuru mkuu wa mkoa wa DSM kwa maandalizi ya mkutano huu na kutoa rai kwa wanahabari kwamba waandike habari za kimaendeleo kama ilivyokuwa kipindi cha baba wa taifa Hayati Julias K. Nyerere alivyotuasa hali itakayopelekea wananchi kupata hatari kujua nini Serikali inawafanyia katika sekta na maeneo mbalimbali.
Sambamba na hilo pia wakurugenzi wote kutoka mkoa wa DSM walielezea kiufupi mafanikio waliyoyapata kwenye majiji yao na kupongeza juhudi zinazofanywa na awamu hii wakieleza 'mambo ni mengi ila muda ni mchache' kuelezea yote, Mkutano huo ulikuwa na kauli mbiu inayosema #TumewasikiaTumewafikia ambapo wakuu wote  wa mikoa ya Tanzania bara watakutana na wakurugenzi wao kujadili mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwenye mikoa yao

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa