• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Nondo 10 za RC Chalamila kwa Wakazi wa Dar

Posted on: August 19th, 2023

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Agosti 19, 2023 ametoa ufafanuzi wa mambo 10 muhimu kwa mstakabali wa maendeleo na ustawi wa jamii katika Mkoa huo na Taifa kwa Ujumla.

RC Chalamila akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake ametoa ufafanuzi na mikakati ya Serikali ya Mkoa kama ifuatavyo:

- Halihalisi ya Uendelezaji wa masoko katika mkoa  RC Chalamila amesema kumekuwa na changomoto kubwa katika Masoko mengi ambapo yako makundi ya watu wachache wasiowaadilifu ambao wanaendesha masoko na Serikali haipati chochote, uamuzi wa Serikali ni kurudisha masoko hayo kusimamiwa na Halmashauri ndio maana hivi karibuni nimevunja uongozi wa Soko la Mabibo hata hivyo tayari timu ya wataalam imeundwa kupita katika masoko yote ya Mkoa na kuleta taarifa ya hali halisi ya masoko hayo

- Migogoro ya Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa na Migogoro mingi ya Ardhi ambayo husababishwa na vikundi vya watu, makampuni ya uuzaji na kupima Ardhi pia kufoji nyaraka mbalimbali tena wengine  wanashirikiana na viongozi wa Umma hili halikubaliki Serikali iko timamu katika kuchukua hatua Stahiki kwa wote wanaochangia migogoro hiyo.

- Usalama wa watu na mali zao Hali ya usalama katika Mkoa iko shwari licha ya kuwa hivi karibuni kulitokea na vijana wachache vingunguti walishazibitiwa na vyombo Mkoa uko salama, "lazima tulinde amani ya Mkoa kwa kuwa ndio kitovu cha biashara, Diplomasia na ni Mkoa wenye watu wengi tusikubali amani itoweke Alisema Mhe Chalamila

- Mabasi yaendayo kasi Rais Mhe Dkt Samia ameendelea kuboresha miundombinu ya usafiri hususani Mwendokasi ameshatoa pesa za kupanua barabara kutoka Ubungo kuungana na njia nane kimara mwisho pia miundombinu imeendelea kuboresha katika maeneo mbalimbali ya Mkoa na sasa Utekelezaji wa awamu ya tatu unaendelea.

- Usambazaji wa Maji kumekuwa na mpango kabambe wa kuboresha miundombinu ya maji ili kuondoa Changamoto ya maji DSM tayari Serikali inajenga bwawa kubwa la kidunda na uchimbaji wa visima vya maji unaendelea Kigamboni na hivi karibuni ataanza ziara ya kukagua miradi ya maji katika mkoa huo.

- Wafanyabishara wadogo machinga kurudi katika maeneo yasiyo rasmi mfano eneo la Mbagala wamekua wakifanya biashara katika miundombinu ya Mwendokasi hivyo amewataka Viongozi wa mchinga kuwahamasisha kufanya biashara kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na si vinginevyo

- Wafanyabishara kulipa Kodi za Serikali kila mfanyabiashara anayetakiwa kulipa Kodi anapaswa kulipa Kodi Serikali imekuwa ikitekeleza miradi mingi ya maendeleo hivyo namna pekee ya kukamilisha miradi hiyo ni kulipa kodi ili Serikali ipate mapato.

-Hali ya migomo migomo isiyo na tija RC Chalamila amesema migomo migomo sio njia sahihi ya kufikia Suluhu za matatizo yetu " ebu jiulize endapo Daktari, Mwalimu au kundi lolote likigoma nini kitatokea? nitoe rai njia ya mazungimzo ni njia sahihi kufikia Suluhu ya matatizo yetu" Alisema Chalamila

-Barabara eneo la Viwanda Kigamboni Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara maeneo mbalimbali ya kimkakati barabara hiyo kuelekea kisarawe II iko katika hatua ya tenda ili ijengwe kwa kiwango cha Lami.

-Usafi RC Chalamila amewataka wakazi wa Mkoa na watu wengine wanaingia na kutoka kila kukicha katika Mkoa huo kuhakikisha Mkoa unakua safi, wafanyabishara, Taasisi na watu wengine kuacha kutupa taka ovyo na amezitaka Halmashauri kutenga bajeti za kuwa na Dampo na kuwalipa wakandarasi wa taka kwa wakati.

Aidha Mhe Albert Chalamila amesema ataendelea kutoa taarifa kwa umma mara mara za utekelezaji wa miradi na mipango ya Serikali kwa masilahi mapana na ustawi wa jamii pia kuanzia mwezi ujao atafanya mikutano mikubwa katika kila Wilaya kueleza Dira na mwelekeo wa uongozi wa Mkoa, kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa