• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Mwarobaini wa kero ya maji Dar es Salaam wakamilika

Posted on: May 4th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda akiambatana na viongozi waandamizi wa Mkoa na Mamlaka ya Maji safi na Maji taka DAWASA wametembelea miradi mikubwa ya uchimbaji wa visima vikubwa 20 vya maji katika maeneo ya Mpera na Kimbiji Wilayani Kigamboni.

Visima hivyo vinavyochimbwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kama njia mbadala ya kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama na kutimiza Sera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kutua ndoo wakina mama wa Tanzania.

Katika ukaguzi huo Mhandisi Alchard Mutalemwa (Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka- DAWASA) alitoa taarifa ya mradi huo wa uchimbaji wa visima 20 (unaogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 370 za kitanzania) ambao umekamilika kwa asilimia kubwa na tayari uchimbaji wa visima 18 umekamilika na utazalisha zaidi ya Lita Milioni 260 za maji kwa siku, huku ikimaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa maji safi katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mhandisi Mutalemwa pia alitoa shukrani kwa Mhe. Paul C. Makonda kwa jitihada zake za kutatua kero ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Mkoa wa Dar es Salaam na kumweleza kuwa ahadi yake aliyoitoa wakati wa ziara ya DAR MPYA mwishoni mwaka jana ya uchimbaji wa visima 10 katika majimbo ya Kibamba na Ubungo  imezaa matunda ambapo  katika majimbo ya Ubungo visima vitano (5) vitachimbwa na jimbo la Kibamba visima vitano (5) ili kupunguza kero kwa wakazi wa majimbo hayo na kuelezea kuwa kukerwa kwake na matatizo ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo kumesababisha kuchukua hatua hiyo.

Uchimbaji huo utaanza karibuni na tayari mkandarasi amepatikana na kazi itaanza mara moja.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda alihoji upatikanaji wa fedha za usambazwaji wa maji yatakayopatikana katika mradi huo wa visima 20 (Mpera, Kimbiji) na kupewa ahadi na Ndg. James Doto Katibu Mkuu wa Fedha aliyeongea nae kwa njia ya simu ya kuwa kama Wizara ya Maji na Umwagiliaji itapeleka ombi la kupatiwa kiasi cha fedha kilichotengwa na bajeti ya Serikali 2016-2017 (Bilioni 44 za miradii ya maji Dar es Salaam) basi fedha hizo zitapatikana na kusaidia usambazaji wa miundombinu ya maji ikiwemo mradi wa visima 20 (Mpera – Kimbiji).

Mradi wa visima 20 (Mpera – Kimbiji) utasaidia usambazwaji wa maji kwa Wilaya tatu za Temeke, Ilala, na Kigamboni na kumaliza kwa asilimia kubwa tatizo la maji Mkoa wa Dar es Salaam.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa