• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam atoa Maelekezo 17 kwa watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi

Posted on: May 18th, 2017


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo 18 Mei, 2017 amezungumza na Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

1.Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi  Kushughulikia migogoro ya Ardhi na Ujenzi ili wananchi wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.

2.Watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja na zoezi hilo lianze mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa Saba kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za Ardhi kwenye mtandao jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani mwa wananchi.

3.Wakuu wa Idara katika Sekta ya Ardhi na Ujenzi  kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana mahusiano na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.

4.Wakuu wa Idara ya Ardhi na Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, na kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.

5.Wakuu wa Idara ya Ardhi Na Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile Shule, Hospitali, na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba na kutoa Mikakati ya Upimaji.

6.Wakuu wa Idara ya Ardhi na Ujenzi kuhakikisha ufanisi na bidii ya utendaji inaongezeka hususani mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka migogoro ya Ardhi.

7.Kushughulikia changamoto za kisera zinazofanya utaratibu wa Upimaji na utoaji wa Hati kuchelewa kukamilka.

8.Mabaraza ya Kata kuangaliwa upya kwa mujibu wa Sheria ili kuwa na utendaji imara unaoshabihiana na jambo la kisera.

9.Kila Mtumishi kufanya kazi yake kwa Uaminifu kwani dhamana aliyopewa ni kubwa na anapaswa kuitendea Haki. Watumishi wote kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani chama hicho ndicho kimeingia mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano.

10.Kila Mkuu wa Idara kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 - 2020 ili kutambua maelekezo yaliyobainishwa katika Sekta yake sambamba na kuwaelekeza wasaidizi wao pia kuisoma na kuielewa vyema Ilani hiyo.

11.Kufatilia na kufahamu upandaji wa madaraja na stahiki zao kwani ni Haki zao za msingi kisheria ikiwa ni pamoja na kwenda likizo.

12.Watumishi wote kuheshimu mamlaka walizonazo na kutumia vikao halali kutoa taarifa sahihi kwa watu husika.

13.Kuwa na ushirikiano wa watumishi katika Idara zote ili kukuza ufanisi wa Kazi.

14.Kujitokeza ndani ya wiki moja kwa watumishi wote wa Sekta ya Ardhi waliojihusisha na utoaji wa Hati za Ardhi kinyume na sheria na endapo wasipojitokeza na wakabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

15.Kufafanua baadhi ya mambo ili Madiwani waweze kuelewa sambamba na kutoogopa maadhimio kama wanatenda kazi kwa mujibu wa Sheria pasipo kupendelea.

16.Wakuu wa Idara kila mwisho wa wiki kutoa taarifa kwa Wakurugenzi inayoonyesha idadi ya Migogoro na jinsi ilivyotatuliwa.

17.Katika kupunguza changamoto ya kuwafikia wananchi kwa Wakati Mkuu wa Mkoa amesema atatoa Pikipiki 5  kwa kila manispaa ya jiji la Dar es salaam, yaani jumla ya pikipiki 25 kwa manispaa zote 5 za Sekta ya Ardhi kwa kila Manispaa.





Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa