• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DAR ES SALAAM KINARA UTOAJI WA HABARI KWA UMMA 2024

Posted on: June 25th, 2024

 

 -RC chalamila apongeza kitengo cha mawasiliano Serikalini kwa kupatiwa tuzo ya ushindi

-Atoa maelekezo mahususi kuboresha utendaji kazi wa kitengo hicho

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 25,2024 amekabidhi tuzo na cheti cha ushindi kwa kitengo cha mawasiliano serikalini kupitia katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt Toba Nguvila tuzo ambayo ilitolewa wakati wa kongamano la sekta ya habari na kikao cha maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanyaika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam Juni 18-22,2024, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Dkt Samia Suluhu Hassan

 

RC Chalamila akikabidhi tuzo hiyo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo ametoa pongezi kwa kitengo cha mawasiliano Serikalini na watumishi wote wa ofisi yake na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa, ambapo amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kukipatia gari na vifaa vya kisasa kitengo cha mawasiliano ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa mkoa Dkt Toba Nguvila amemuhakikishia mkuu wa mkoa kuendelea kusimamia wataalam katika mkoa huo kwa weledi mkubwa ili kuwa na utumishi wenye tija kwa mkoa na Taifa kwa ujumla.

Aidha tuzo na vyeti hivyo wakati wa kongamano la sekta ya habari vilitolewa katika makundi manne (4), kundi la Wizara kwa wizara 10, Kundi la Mamlaka za Maji 10, kundi la Mikoa 10 na kundi la Wilaya 20 zilizofanya vizuri ambapo Mkoa wa Dar es Salaam umeibuka kinara kwa kishika nafasi ya kwanza(1) kati ya mikoa yote ya Tanzania bara kwa kufanya vizuri katika kutoa habari kwa Umma.

Pia Mkoa wa pili (2) ni Mwanza, tatu (3) Arusha, nne(4) Dodoma, tano(5) Ruvuma, sita(6) Pwani, saba(7) Morogoro, nane(8) Kilimanjaro, tisa(9) Tanga na Mkoa wa kumi(10) Njombe.

Sanjari na hilo katika kundi la Wilaya bado Dar es Salaam imefanya vizuri ambapo Wilaya ya Temeke imeshika nafasi ya kwanza (1), Ilala nafasi ya 4, Ubungo ya 5, Kinondoni ya 17 na Kigamboni nafasi ya 20 kati ya Wilaya zote za Tanzania bara.

Mwisho hafla ya makabidhiano ya tuzo na cheti ilihudhuriwa na wakuu wa idara na vitengo, watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa makao makuu na watumishi wengine kutoka katika wilaya zote za mkoa huo.

 

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa