• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

MHE. Samia Suluhu Hassan: Kila siku iwe ni siku ya Kuhifadhi na Kutunza Mazingira

Posted on: June 5th, 2018

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa ngazi zote kuongeza nguvu katika utekelezaji wa Sera, Sheria, Mikakati na Miongozo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja.

“ Ni muhimu, mipango ya maendeleo katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ili nchi yetu iwe na maendeleo endelevu” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kazi ya kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Uhifadhi wa Mazingira inahitaji ushirikiano wa wadau wote kwa ngazi zote.

Ameongeza kuwa  watanzania wanapaswa kuelewa athari zitokanazo na ukataji wa miti kiholela na kuhakikisha wanakuwa walinzi wa kwanza wa Mazingira hayo.

Amezitaja athari hizo kuwa ni kukimbiza wanyama, kupoteza matunda ya asili, kuharibu makazi ya wadudu wenye kazi mbalimbali, kuharibu misitu inayotusaidia kunyonya joto au hewa ukaa na bahari kuingia eneo la makazi ya watu.

Maadhimisho ya Kimataifa yanafanyika India katika mji wa New Delhi yakibeba ujumbe wa kuhimiza kupunguza uchafuzi wa Mazingira kutokana na matumizi ya bidhaa za plastiki (Beat Plastic Pollution) lakini hapa nchini Kitaifa ujumbe wa maadhimisho ni “Mkaa Gharama: Tumia Nishati Mbadala”.


Awali, Makamu wa Rais alizindua ukuta wa bahari uliopo kwenye barabara ya Barack Obama wenye urefu wa mita 920, ukuta huo ambao umejengwa kuzuia bahari kuingia nchi kavu unakadiriwa kuwa na maisha kati ya miaka 70 mpaka 100 kutoka sasa.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa Viwanda na zipo faida nyingi za hifadhi na usimamizi zitakazotokana na Tanzania kuwa na Viwanda.

Akitoa Salamu za Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ametangaza kuanza kwa oparesheni kabambe ya kuwakamata na kuwatoza faini wachafuzi wa Mazingira kuanzia July Mosi kwa lengo la kuhakikisha jiji linakuwa kwenye Hali ya usafi kama majiji mengine ulimwenguni.

RC Makonda amesema ameandaa vijana zaidi ya 4,000 kutoka Jeshi la kujenga Taifa JKT ambao watafanya kazi ya kuwakamata watupaji wa taka barabarani na mitaani.

Vijana hao 4,000 ni wale waliomaliza mafunzo ya JKT na hawana kazi ambapo RC Makonda ameamua kuwachukuwa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo na kwenye kiasi cha faini watakazo watoza wachafuzi wa mazingira 40% itaenda kwa vijana hao na 60% itaingizwa Serikalini.

Aidha RC Makonda amesema hawezi kukubali kuona Jiji linakuwa kwenye hali ya uchafu wakati ipo sheria ya mwaka 2004 inayotoa mamlaka ya kuwawajibisha wananchi wenye tabia kuchafua mazingira kwa makusudi.

Itakumbukwa kuwa kila mwaka viongozi wamekuwa wakihimiza usafi na hata alipokuja Rais Barack Obama miaka kadhaa iliyopita barabara zilipigwa deki na alipoondoka uchafu ukaendelea na hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli alifanya usafi Kama sehemu ya kuhimiza usafi lakini bado watu wamekaidi, pia ulianzishwa utaratibu wa usafi kila jumamosi watu wasifungue maduka hadi wafanye usafi lakini bado pia wamekaidi jambo ambalo RC Makonda ameamua sasa kuja na mkakati wa kuwatumia vijana wa JKT wasiokuwa na kazi  kufanya jukumu la kuwakamata wachafuzi wa mazingira.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa