• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru

Posted on: June 1st, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul C. Makonda amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo mapema leo asubuhi baada ya kukaa ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam  kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 27/05/2017 mpaka tarehe 31/05/2017

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Wahe. Madiwani, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam, Makatibu Tawala wa Wilaya zote, Wadau mbalimbali wa Maendeleo, Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa na Vikundi vya Hamasa vya Mkoa wa Dar es Salaam.

Awali, Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alianza  kwa kumshukuru Mungu na kuwakaribisha wote waliofika kwa ajili ya tukio muhimu la makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.

Katika hotuba yake Mhe. Paul Makonda alieleza jinsi Mwenge wa Uhuru ulivyotimiza azma yake kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kukagua miradi yenye thamani ya Tshs 244,392,530,334/= ambapo miradi mikubwa 12 ilizinduliwa, miradi 5 iliwekewa mawe ya msingi, na miradi 11 ilitembelewa na kufunguliwa.

Mhe. Paul  Makonda alieleza kuwa aliupokea Mwenge wa Uhuru ukitokea katika Mkoa wa Lindi na umefanya mambo mengi makubwa na mazuri kwa Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo ameukabidhi Mwenge huo kwa Mkoa wa Pwani kwa moyo mweupe ili ukazindue, kutembelea na kuweka Mawe ya Msingi katika Miradi mbalimbali Mkoani humo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kuwa ameupokea Mwenge wa Uhuru na ameahidi kuukimbiza katika Wilaya zote saba zilizopo katika Mkoa huo sambamba na kuzindua, kutembelea na kuweka Mawe ya Msingi katika Miradi itakayogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni themanini na tano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Dar es Salaam zimekua kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja, Mshikamano na Kudumisha Amani.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa