• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Maelfu ya Wakazi wa DSM Wajitokeza Kuadhimisha Siku ya Amani Duniani

Posted on: September 28th, 2024

 

-RC Chalamila asema bila Amani ni vigumu kufanikisha malengo ya maendeleo.

Maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wamejitokeza kwa wingi Leo Septemba 28, 2024 kuadhimisha siku ya Amani katika Viwanja vya Mwembe yanga jijini humo.

Akihutubia wananchi waliojitokeza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila amesema kila ifikapo tarehe 21 Septemba Dunia huadhimisha maadhimisho ya siku ya Amani duniani kutokana na uingiliano wa ratiba Mkoa unaadhimisha maadhimisho haya Leo Septemba 28,2024.Siku hii ni muhimu kwakuwa ina kumbusha watu kuhusu umuhimu wa kutatua migogoro kwa njia za amani,kuzuia vita, kuimarisha mshikamano na umoja miongoni mwa jamii.

Vilevile ni fursa adhimu ya kuangazia maswala ya haki, usalama na maendeleo endelevu ili kujenga Taifa bora kwa Kila mtu .

Aidha RC Chalamila amesema ni muhimu kulinda na kudumisha Amani tuliyonayo,bila Amani ni vigumu kufanikisha malengo ya maendeleo.

Sambamba na hilo RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta 4R ikiwemo maridhiano kama nguzo ya amani katika Nchi yetu pia, ameelezea lengo la maadhimisho hayo ni kutoa fursa ya kuhamasisha watu kujenga uelewa juu ya maswala ya amani, umoja na ushirikiano.

Katika maadhimisho hayo viongozi wa dini walipata wasaa wa kuzungumza na kutoa nasaha kwa wananchi hasa kwenye maswala ya kudumisha Amani kwenye Taifa letu ambapo Shekh Yahaya ambaye ni muwakilishi wa mashekhe wa Mkoa wa Dar es salaam ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kusimama kidete na kuonesha hekima na busara  kuilinda nchi iendelee kuwa na Amani hususani Mkoa huu jambo ambalo limeungwa mkono na viongozi wengine toka madhehebu mengine.

Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Toba Nguvila wakati anamkarbsha mgeni rasmi Mhe. Albert Chalamila amesema nia ya maadhimisho hayo ni kuimarisha amani katika Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na hata kusaidia kutatua migogoro katika jamii kwa kuwa wamoja hususani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa mwezi Novemba 27,2024.

Mwisho, Licha ya wananchi wengi kujitokeza katika maadhimisho hayo viongozi mbalimbali wamejitokeza pia, ikiwemo Wakuu wa Wilaya,wastahiki meya , Wakuu wa Taasisi, Makatibu Tawala wa Wilaya zote tano ,viongozi wa dini, wazee na watu mashuhuri na kupambwa na burudani kadha wa kadha kutoka kwa waimbaji wa nyimbo za injili kama vile Bahati Bukuku na makundi maalumu yaliyosherehesha kwa kiwango kizuri

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiwasili NIDC-Kijitonyama

    May 15, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Charles Hilary

    May 13, 2025
  • Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa yakagua Miradi ya Maendeleo Wilaya ya Temeke

    May 07, 2025
  • RC Chalamila Aongoza Maadhimisho ya Mei-Mosi Dar es Salaam.

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa