• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Ngazi ya Mkoa

Posted on: June 5th, 2017

HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MHE. PAUL C. MAKONDA KATIKA KILELE CHA MADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI NGAZI YA MKOA

VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, TAREHE 05/06/2017

 

Katibu Tawala wa Mkoa,

Wah. Wakuu wa Wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke,

Wah. Mameya

Wah. Madiwani

Wakurugenzi wa Halmashauri,

Watendaji wa Serikali, 

Wadau wote wa Mazingira 

Wageni waalikwa, 

Mabibi na Mabwana.

Ndugu Wananchi,

Leo hii tunaungana na Wenzetu Duniani kote kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani. Siku hii huadhimishwa kila mwaka tarehe 05 ya mwezi Juni, Duniani kote. Lengo kuu la Maadhimisho ya siku ya Mazingira mwaka huu ni kufanya tathmini ya Mazingira, kubaini changamoto zinazoikabili Sekta ya Mazingira na kutoa mwelekeo wa kupambambana na changamoto hizo ili kuwa na Mazingira bora na endelevu.

Ndugu Wananchi, 

Mwaka huu Maadhimisho ya Kitaifa hapa nchini yanafanyika Mkoani Mara katika kijiji cha   Butiama    ili kumuenzi hayati Mwalimu Julius Nyerere katika dhana ya kuhifadhi mazingira.   Kauli mbiu ya Mwaka huu Kitaifa ni ″Hifadhi ya Mazingira; Mhimili kwa Tanzania ya Viwanda‶. Kimataifa ni ″Mahusiano endelevu kati ya Binadamu na Mazingira‶. (″Connecting People to Nature‶.)

Ndugu Wananchi,

Maadhimisho haya hutanguliwa na shughuli mbalimbali zinazohamasisha utunzaji mazingira ambazo hufanyika katika maeneo mbalimbali kuelekea siku ya kilele.  Kwa wiki hii ya maadhimisho, Halmashauri za Manispaa zimepanda jumla ya miti 10,747 katika maeneo ya wazi, mabondeni, mashuleni na pembezoni mwa barabara. Pia usafi umefanyika kwenye maeneo ya mifereji, masoko na fukwe. Shuguli hizi zimeambatana na ukaguzi wa vifaa vya makampuni ya usafi na uhamasishaji wa wananchi katika masuala ya uhifadhi na usafishaji wa mazingira yanayowazunguka.  Kwa mkoa wa Dar es Salaam shughuli hizi zilianza tangu tarehe 31/05/2017 na leo hii ndiyo tumefikia siku ya kilele cha Maadhimisho haya.

Ndugu Wananchi,

  • Tunatambua kuwa Mkoa wetu unakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi kama ilivyo kwa nchi nzima na dunia nzima ambazo asilimia kubwa zimetokana na shughuli za kibinadamu.   Athari hizo vile vile huambatana na milipuko ya magonjwa ya mara kwa mara kwa binadamu, mifugo na kilimo, kuharibika kwa mifumo ya ikologia inayotokana na kuongezeka kwa hali ya joto, kuongozeka kwa maji ya bahari na kusababisha kuzama kwa baadhi ya visiwa vyetu na kumomonyoka kwa kingo za bahari.  Pia kumekuwa na mvua zisizotabirika ambazo zimesababisha mafuriko na ukame kwenye maeneo mengine na zimeathri sekta za Kilimo, Mifugo, uvuvi, Usafirishaji, Makazi, Miundombinu hali ambayo inaathari moja kwa moja mipango ya uchumi na maendeleo ya Mkoa wetu na nchi kwa ujumla.

Licha ya changamoto hizo, zipo pia changamoto za kimazingira ambazo zinatokana na ukiukwaji wa sheria kunakosababishwa na wananchiukiukwaji huo ni kama utupaji taka ovyo, utiririshaji maji machafu, uchimbaji holela wa mchanga, vifusi na kokoto, ukataji miti holela, biashara kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi na ujenzi holela katika maeneo hatarishi hususani wa mabondeni na kwenye vyanzo vya maji.

Ndugu Wananchi,

Ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi pakiwemo na za Kimazingira, Serikali tumeanzisha miradi mbalimbali katika maeneo mbalimbali ya Halmshauri zetu kwa kutumia mapato ya ndani, wadau wa maendeleo na mifuko ya fedha ya kimataifa kwa uborashaji wa miundo mbinu, miradi mbalimbali na mifumo ya ikologia.  Miradi hii inahusha na ujenzi wa kingo za bahari, mifereji ya maji ya mvua, uboreshaji wa barabara, upandaji wa mikoko, ukarabati wa matumbawe, upandaji miti, ukarabati wa mwambao wa bahari, na uthibiti wa uvuvi haramu, Vilevile juhudi zimendelea kwa na kukuza uelewa wa matumizi endelevu ya rasilimali   kwa wadau na vikundi vya kijamii, kuhusiana na sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara ili kuimarisha uhifadhi wa mazingira.

Vilevile kupitia kwa wataalam wa mazingira Halmashuri zetu zinawajibika kudhibiti miradi na viwanda chafuzi kwa mazingira, kwa kusimamia tathmini na hakiki za Athari kwa Mazingira, ukaguzi wa viwanda na kuhakikisha miradi yote inayoanzishwa inakuwa na mipango ya kusimamia mazingira. Uhifadhi wa mazingira ukipewa umuhimu unaostahili tutaweza kupambana na uharibifu wa mazingira na kusababisha changamoto zitokanazo na umasikini, maradhi, hali mbaya na duni ya upatikana chakula, makazi duni, maji yasiyo salaama na upatikanaji wa nishati usioridhisha na kusambaa holela kwa mji.

 Ndugu wananchi,

 Suala la taka ngumu na usafi wa mazingira limekuwa na   changamoto katika Mkoa wetu. Inakadiriwa kwa sasa Mkoa huu una watu zaidi ya milioni 5 na viwanda vikubwa na vidogo vipatavyo 1,885 ambapo kwa pamoja huzalisha taka tani 4,500 kwa siku, takiribani asilimia 50 ya taka zinazo zalishwa huzolewa na kupelekwa kwenye kituo cha kutupia taka (dampo) na asilimia 50 hubaki mitaani kutokana na uwezo mdogo wa Halmashauri. Inakadiriwa kwamba asilimia 70 ya taka zinazozalishwa ni za kuoza (organic waste) ambazo zina athari kubwa zikiachwa kwenya mazingira. Kutokana na hali hii mkoa unao mpango wa kuanzisha kiwanda cha kuchakata taka na kuwa mbolea ambapo wakulima wa Dar es salaam watajengewa uelewa na kuhamasishwa kutumia mbolea inayotokana na taka hizo na mpango huu utapunguza kiwango cha taka zinazobaki mitaani.

Ndugu Wananchi

Kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu, ni dhahiri kwamba imebeba ujumbe kamili wa kumuunganisha mwananchi na Mazingira asilia yanayomzunguka (Connecting People to Nature); inatoa mwanya kwa wakazi wote wa Mkoa wetu kutafakari upya kama shughuli wanazozifanya zinazingatia utunzaji wa Mazingira endelevu na yenye tija kwa ajili ya Maendeleo ya sasa na ya baadaye.

Ndugu Wananchi,

Kutokana na changamoto zinazo tukabili nasisitiza kuwa Sheria ya Mazingira, sheria za kisekta na Sheria Ndogo zilizopo zinazohusiana na usafi na utunzaji wa Mazingira zitumike inavyopaswa ili kuondoa utupaji taka ovyo, utiririshaji maji machafu na mchimbaji holela wa mchanga, vifusi na kokoto, ukataji miti holela, biashara kwenye maeneo yasiyokuwa rasmi na ujenzi holela hususani wa mabondeni na kwenye vyanzo vya maji.

Nasisitiza kuwa ni wajibu wa Watendaji wote waliopewa dhamana na Serikali wanawajibu wa   kulinda na kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira katika maeneo yao.  Natoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoa ushirikiano wa dhati ili kuunga mkono juhudi na mikakati ya kutunza na kuhifadhi mazingira kwani mazingira ndio urithi kwa vizazi vya baadaye.

Mwisho naomba Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano za kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda; kuongoza mapambano dhidi ya madawa ya kulevya; kuhimiza usafi wa mazingira na kuondoa utoroshaji wa rasilimali za nchi.

Nachukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote wa kutoka taasisi za umma na za binafsi mnaoshirikiana nasi katika masuala yote yanayohusiana na mazingira. Ninawaomba mwendelee kuiunga mkono Serikali yenu kwa kuyatunza, kuyalinda na kuyahifadhi Mazingira yetu.

Kwa mara nyingine nawashukuru wananchi wote, kwa kujitokeza kwa wingi siku hii ya leo kwa ajili ya kuadhimisha siku hii muhimu duniani   

ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa