• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

KATIBU TAWALA AKUTANA NA WACHUMI, WAKUU WA VITENGO VYA TEHAMA NA MAAFISA HABARI

Posted on: September 2nd, 2017

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando amefanya kikao na Wachumi, Wakuu wa Vitengo vya TEHAMA na Maafisa Habari katika Mkoa wa Dar es Salam.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Ilala na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Makatibu Tawala wa Wilaya.

Akifungua mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa amesema kikao hichi ni muhimu ambapo kinawaunganisha wataalamu wa sekta hizo kuzungumzia namna ya kuboresha utendaji wa kazi za kila siku.

Amesema nimewaita kada tatu tofauti nikiamini kuwa kila mmoja anatekeleza majukumu yake lakini ipo haja ya kuwa na uhusiano wa ukaribu katika  utendaji wa kazi zenu kwani Maafisa Habari wanapaswa kuandika habari za ukweli na uhakika zinazotoka katika Idara ya Uchumi zinazoelezea uwepo wa shughuli za maendeleo ya kiuchumi na uwekezaji katika Mkoa wetu.

Aidha Katibu Tawala amewataka Maafisa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwani kuna mambo mengi yanafanywa katika mkoa wetu lakini hayafiki kwa  wananchi. Amewataka kutumia REDIO YA JIJI inayoitwa CITY FM yenye masafa ya 91.7. Amesema “Tunayo Redio yetu ya Jiji ambayo tunapaswa kuitumia kikamilifu kwa kuelezea yaliyomo katika Mkoa wetu kwani tunazo shughuli nyingi zinafanyika lakini hazisikiki”. Tupange utaratibu mzuri na endelevu wa  kwenda katika RADIO YA JIJI angalau siku moja moja kutoka katika Halmashauri zetu na Mkoa ili kuelezea yaliyomo katika sehemu/maeneo  yetu.

Kwa upande wa Makatibu Tawala wa Wilaya nao pia washaurianae na Halmashauri za Manispaa zao mambo yafuatayo:-

Wachumi kuwapatia Maafisa Habari taarifa zinazotoka katika sehemu zao kwani kuna mambo mengi sana yapo na hawajayatoa bado kwa wananchi.

Aidha, ilishauriwa wajitahidi kukuza ushirikiano kati yao na Maafisa Habari kwani itawarahisishia kufikisha taarifa kwa wananchi kwa urahisi.

Kwa upande wa Maafisa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam walikubali na kuazimia kuwa kuanzia sasa na kuendelea watafanya mapinduzi makubwa ya kihabari kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.Waliahidi kutumia REDIO YA JIJI ipasavyo sambamba na kuanza sasa kuandaa Makala, Vipeperushi, Majarida na Documentary mbalimali.

Katibu Tawala wa Mkoa alimaliza kikao chake kwa kuwataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwani kila mmoja akitimiza wajibu tutapunguza kero ambazo wananchi wanailalamikia Serikali yao.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa