• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Halmashauri Dar, Zatakiwa Kutumia Jeshi la Akiba.

Posted on: August 15th, 2025

 

MKUU wa Wilaya  ya Temeke, Mhe Sixtus Mapunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amezielekeza Halmashauri ya Jiji  na Manispaa zote Mkoani humo kuhakikisha zinawatumia kikamilifu  wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba katika utekelezaji wa operesheni mbalimbali.

Ametoa maelekezo hayo leo Agosti 15, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe  Albert Chalamila, katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba  Kundi  la 63/2025 yaliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi la Wanamnchi Tanzania ya  Twalipo, wilayani Temeke.

“Halmashauri zote katika shughuli zao na operesheni zao ziwatumie  vijana hawa, Wakurugenzi muwatumie wahitimu hawa  haraka kabla hawajarudi mtaani,” amebainisha  Mapunda ambapo amesema  vijana hao wakiachwa  mtaani kwa kipindi kirefu  bila kutumika  watasahau kwa haraka kiapo chao.

“Tuna operesheniu za kukusanya mapato. Tuna maandalizi ya uchaguzi mkuu na kusimamia taratibu mbalimbali katika Halmashauri zetu.

"Hawa vijana  wako tayari kutumika,”ameeleza Mapunda.

Aidha, ametoa  wito kwa wahitimu hao  kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu pia ametoa rai siku ya uchaguzi mkuu kujitokeza kwa wingi kupiga kura, "ninawakabidhi jukumu la kwenda  kuhamasisha vijana wenzenu kujitokeza kupiga kura,” amesema.Mapunda

Vilevile amewataka, wahitimu hao kuishi kiapo walicho apa na kujiepusha kutumia mafunzo waliyopata  katika vitendo viovu.

Kwa upande wa Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Emmanuel Kasyupa, alisema mafunzo hayo  yalijumuisha vijana kutoka wilaya tano za Mkoa huo ambazo ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo, mafunzo  yalianza April nne mwaka huu yakiwa na wanafunzi 414. wanafunzi 66 walishindwa kuendelea kutokana na sababu  mbalimbali zikiwemo za utoro, matatizo ya afya na utovu wa nidhamu aidha jumla ya wahitimu wote ni 348, wanaume  263  na wasichana 85 ambapo mafunzo hayo yalifanyika kwa wiki 18.

Hata hivyo Kanali Kasyupa amebainisha, wakufunzi wa mafunzo hayo walitoka katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

 “Kiapo kimesikika Mmeahidi kuwa watiifu na waaminifu  kwa Amiri Jeshi Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtakuwa watiifu kwa raia . msiende kukiweka  kiapo hiki katika begi ikiwezekana bandikeni sebuleni ili mgeni akija atambue unawajibu gani kwa Taifa,”.

Sambamba na hilo amesisitiza  wahitimu hao  kulinda  uhuru na uchumi  wa Nchi kama walivyo apa.kwa kuwa Askari hao wamefikia kiwango kinachokubarika  katika Jeshi la akiba na wapo tayari kutumikia  taifa katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

Ifahamike kuwa katika mafunzo hayo wahitimu hao walipata masomo mbalimbali kwa nadharia  na vitendo, ikiwa ni pamoja na kwata, ukakamavu, mbinu za kivita, ujanja wa porini, usomaji ramani, huduma ya kwanza, zimamoto, uhamiaji, usalama wa taifa, kuzuia na kupambana na rushwa , silaha ndogondogo, utimamu wa mwili, uraia, kazi za polisi, ,Sheria za Jeshi la Akiba, na vita vya  msituni.

Mwisho, katika risala yao  wahitimu hao waliiomba Serikali kuongeza bajeti ya mafunzo ya jeshi la akiba na kuwapa kipaumbele  kujiunga na JKT  na  taasisi zingine za Serikali

Matangazo

  • DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 July 17, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA WA DARASA LA SABA MEI, 2025 July 18, 2025
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RAS MHINTE ASISITIZA MAMBO MATATU KUZINGATIWA NA SEKRETARIETI YA MKOA, WAKURUGENZI NA WAKUU WA SEHEMU NA VITENGO WA HALMASHAURI

    August 18, 2025
  • Halmashauri Dar, Zatakiwa Kutumia Jeshi la Akiba.

    August 15, 2025
  • Wabunge wa Bunge la Taifa Korea Watembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

    August 12, 2025
  • RC Chalamila Atembelea na Kukagua Mabanda ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki 2025

    August 06, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa