• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

DC Hapi : Asisitiza umuhimu wa upandaji wa Miti katika Maadhimisho ya Wiki ya upandaji wa Miti Kimkoa

Posted on: April 6th, 2018

Maadhimisho ya wiki ya upandaji miti ngazi ya Mkoa, yameadhimishwa katika Manispaa ya Kinondoni kwa kupanda takriban miti 800 kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa huo ,kutoka katika vitalu vya wakala wa misitu (TFS) kwa kushirikiana na Halmashauri za Mkoa wa Dar es salaam.

Akiongea katika maadhimisho hayo, yaliyofanyika katika Kata ya Kunduchi, Manispaa ya Kinondoni, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mh. Alli Hapi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amesema siku hii ni muhimu sana kwa wananchi kushiriki ili kwa pamoja tuweze kufikisha ujumbe mahususi kwa jamii kuhusiana na umuhimu wa upandaji miti, utunzaji na usimamizi wake.

"lengo ni kutumia siku hii maalum kufikisha ujumbe kwa jamii yetu, juu ya kuihamasisha Jamii katika swala zima la upandaji miti, utunzaji na usimamizi wake, na matumizi endelevu juu ya rasilimali zetu za misitu. "Amesema Hapi

Akifafanua kuhusiana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo "Tanzania ya Kijani inawezekana panda miti kwa Maendeleo ya viwanda" amesema ni muhimu Sana Tanzania yetu ya viwanda ikaendana na zoezi la upandaji miti kwani kwa kufanya hivyo itapunguza uharibifu wa tabaka la juu la anga (ozone) itokanayo na uzalishwaji wa hewa ya ukaa, ambapo uharibifu unapotokea husababisha miale ya moja kwa moja kushuka na kuumiza viumbe hai.

Ameongeza kuwa upandaji wa miti na utunzaji wa Mazingira ni ajira nzuri kwa vijana, kwani Mazingira yawapo mazuri na safi huwa vivutio kwa watu kupumnzika na kufanya shughuli zao .

Aidha amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam kuweka mifumo ya maji katika barabara zilizopandwa miti ili kuweza kurahisisha umwagiliaji.

 Awali akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, mwakilishi wa wakala wa huduma za  misitu nchini (TFS)  Bi Dyaga Follen Mkomwa, amesema siku hii ya upandaji miti kitaifa inatokana na waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 2000 ,ambapo kila Wilaya nchini inatakiwa kupanda miche ya miti milioni moja na laki tano kila mwaka.

Ameongeza kuwa misitu iliyopo katika Mkoa wa Dar es salaam pamoja na upandaji huu wa miti ni jitihada za viongozi mbalimbali wa Serikali katika kusimamia utunzaji Mazingira, ambayo inasaidia kuboresha Mazingira na kufyonza hewa ukaa inayozalishwa viwandani kwa sasa, na pia kukabiliana na ongezeko kubwa la hewa ukaa itakayozalishwa kutokana na mkakati uliopo wa kuongeza viwanda katika Mkoa wa Dar es salaam.

Maadhimisho haya kimkoa yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali kutoka katika Halmashauri zote za Mkoa wa Dar es salaam,  ambapo Kitaifa yanadhimishwa mkoani Shinyanga katika wilaya ya Kishapu.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Temeke Yang'ara Mwenge wa Uhuru 2025

    June 02, 2025
  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa