• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Dar Yatoa Msaada wa Vifaa Mbalimbali kwa Wahanga wa Mafuriko Hanang- Manyara

Posted on: December 6th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila, leo Desemba 6, 2023 ametoa Salamu za pole na msaada wa vifaa mbalimbali kwa waathirika wa maafa ya mafuriko Wilaya ya Hanang Mkoa wa Manyara.

Akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa kutoa vifaa hivyo RC Chalamila amesema  viongozi wote wa wilaya za Mkoa wa DSM na wadau wanaungana na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa pole na kuwasitiri wahanga wote wa mafuriko kwa kutoa vifaa mbalimbali vikiwemo magodoro 250, mablanketi ya wakubwa 1200 na ya watoto 300, sabuni  katoni 100, mikeka 500, ndoo ndogo ( Lt 10) 350 na kubwa (Lt 20) 350, sahani 500 na seti za kupikia 20.

"Tunatoa pole kwa watanzania wenzetu ambao wamefikwa na maafa hayo, sisi wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mimi Mkuu wa mkoa tunaungana pia na viongozi wa Mkoa wa Manyara na hasa hasa kumpa pole za dhati kabisa Mhe Queen Sendiga ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara," alisema RC Chalamila

Vilevile RC Chalamila amesema majanga yaliyotokea Hanang yachukuliwe kama somo na yanaweza kutokea sehemu yoyote, hivyo alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam kuendelee kuchukua tahadhari, kuhama  mabondeni, kufungua njia za maji, kufanya usafi ili kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Pia Mhe Chalamila amesema mkoa wa DSM ni mji muhimu kwa mengi ikiwemo biashara, diplomasia, na uchumi hivyo tatizo lolote likitokea litagharimu maisha ya wengi, "Natoa wito kwa wakazi wa DSM kuilinda DSM kama mboni ya jicho kwa maslahi mapana ya taifa letu," alisisitiza.

Mwisho ikumbukwe kuwa Desemba 3 mwaka huu wakazi wa Hanang walikubwa na mafuriko ya maji yaliyoambatana matope, mawe na magogo na kusababisha vifo na majeruhi kwa watu na mifugo, na uharibifu wa miundombinu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Rais wa Finland Alexander Stubb Atembelea Machinga Complex - DSM

    May 16, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa