• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Dar Sasa Kuwa Kama Busan

Posted on: June 16th, 2023

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Said Kumbilamoto na Mstahiki Meya Park Heong Joon, Meya wa Jiji la Busan la Korea Kusini wametia saini Mkataba wa kuwa na Uhusiano wa Kidugu (Sistership Relations) baina ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Busan.

Utiaji saini umefanyika Jijini Busan Korea Kusini tarehe 15 Juni 2023 kwenye Hoteli ya Western Josun.

Jiji la Busan ni la pili kwa ukubwa hapa Korea. Bajeti yake kwa mwaka ni Dola bilioni 10 sawa na Trilioni 23 za kitanzania, ambayo ni nusu ya bajeti ya nchi yetu. Jiji hili lina mahusiano na majiji makubwa 23 katika nchi 26 duniani. Barani Afrika lina mahusiano na majiji ya Western Cape (South Africa), Rabat (Morocco) na Algiers (Algeria).

Jiji la Busan ndio lenye bandari ya lojistiki ya pili kwa ukubwa duniani na bandari ya tano kwa ukubwa ya makontena duniani. Ndio jiji lenye viwanda vya ujenzi wa meli nchini Korea, sekta ya uvuvi na viwanda vya uvuvi. Pia ni jiji la pili kwa sekta ha filamu nchini Korea. Ndio jiji linalotarajiwa kuwa mwenyeji wa Maonyesho ya Biashara ya Dunia (World Expo) iwapo watashinda kinyang'anyiro cha kuwa wenyeji kwa mwaka 2030.

Kufuatia mazungumzo ya awali na katika kuonyesha nia njema, Jiji la Busan tayari limesaini MoU na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya kusaidia uendelezaji wa sekta ya filamu.

Pichani ni Viongozi wa Jiji la Busan na Dar es Salaam wakionesha nakala za Mikataba waliyotia Saini kuanzisha rasmi  ushirikiano wa Kidugu

Baada ya utiaji saini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila aliyeongoza Ujumbe wa Jiji la Dar es Salaam kwenye ziara ya Siku 4 nchini Korea ameelezea hatua hiyo kuwa ya kimkakati itakayofungua fursa mpya za ushirikiano baina ya Majiji yetu Mawili kwenye sekta muhimu za Maendeleo, Biashara, Uchumi na Ustawi wa Jamii

Akizungumzia kuhusu Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa  Meya Park wa Jiji la Busan ameeleza kuwa Jiji lake Lipo tayari kushirikiana na Jiji la Dar es Salaam kwenye kujengeana uwezo, kupeana fursa za mafunzo kwa watumishi, ujenzi wa miradi ya maendeleo, uboreshaji wa miundombinu, nishati, sanaa, filamu, udhibiti wa taka na utunzaji wa mazingira

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Said Kumbilamoto, Bw. Amani Ibrahim Mafuru na Bi Theresia Dennis Mwakasungula wa Mamlaka ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Bwana Abilah Namwambe wakiwa kwenye  picha ya pamoja na uongozi wa Mamlaka ya jiji la Busan

Akiwa Korea Mheshimiwa Chalamila na ujumbe wake wamezuru Taasisi mbalimbali za Jiji la Busan kujionea utendaji kazi na uratibu wa majukumu mbalimbali ya kimaendeleo

Akizungumzia kuhusu Ushirikiano huu  Bw. Namwambe Afisa Ubalozi wa Tanzania Korea Kusini ameeleza kuwa hatua hii ni matunda ya juhudi za Ubalozi za kuhamasisha na kukuza  ushirikiano wa taasisi za serikali,  sekta binafsi na kukuza ushirikiano wa watu na watu baina ya Tanzania na Korea ili kurahisisha utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa