• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Dar - Kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Machi 17- 23,2025

Posted on: March 5th, 2025

 

-Wapiga Kura wapya zaidi ya Laki sita wanatarajiwa kuandikishwa na Tume. 

Mkoa wa Dar es Salaam unatajia kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuanzia tarehe 17 hadi 23 Machi 2025 ambapo wapiga kura wapya 643,420 wanatarajiwa kuandikishwa. Hayo yamesemwa leo Machi 5, 2025 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhan kwenye mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

“Leo tupo hapa Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa huu, ambapo zoezi litafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe 17 Machi, 2025 na kukamilika tarehe 23 Machi, 2025 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele.

Amesema Mkoa wa Dar es Salaam ndio wa mwisho kwenye awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Dafatri ambayo ilizinduliwa mwezi Julai, 2024 mkoani Kigoma ambapo mpaka sasa zoezi hilo limeshafanyika kwenye mikoa 28 na kwamba mikoa ya Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga inatarajiwa kukamilisha zoezi hilo tarehe 07 Machi, 2025.

“Hadi leo tarehe 05 Machi, 2025 Tume imeshakamilisha uboreshaji wa Daftari katika Mikoa 28. Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 13 ambao ni mzunguko wa mwisho wa uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu unahusisha Mkoa wa Dar es Salaam pekee.

Aidha, zoezi la uboreshaji wa Daftari kwenye mkoa wa Morogoro na sehemu ya mkoa wa Tanga kwenye Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli, Handeni, Pangani na Mkinga unaendelea tangu tarehe 01 Machi, 2025 na utakamilika tarehe 07 Machi, 2025,” amesema Jaji Mwambegele. Akiwasilisha mada kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu. Kailima Ramadhan amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 643,420 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 3,427,917 waliopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. “Tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na wapiga kura   4,071,337. Aidha, idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha,” alisema Kailima.

Sanjari na hilo Mkoa wa Dar es Salaam una vituo    1,757   vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo      96     katika vituo         1,661    vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Vilevile Kailima amesema zoezi la uboreshaji wa Daftari linahusu kuandikisha wapiga kura wapya ambao ni raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kutoa kadi mpya kwa wapiga kura waliopoteza kadi au kadi zao kuharibika na kutoa fursa kwa wapiga kura walioandikishwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine. “Uboreshaji wa Daftari pia utahusu kutoa fursa kwa wapiga kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa wapiga kura waliopoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wa Tanzania na kifo,” amesema Kailima

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Ukatili Kinara Migogoro inayohitaji Msaada wa Kisheria-Waziri Mkuu

    June 16, 2025
  • Wananchi Dar Kunufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia

    June 14, 2025
  • RC Chalamila, Samia Legal Aid Kuzinduliwa Juni 16, 2025 DSM

    June 13, 2025
  • Wataalam Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Wakutana na Kamati ya Usalama ya Mkoa-DSM

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa