• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Dar es Salaam Yafanya Mafunzo ya Siku 2 ya Kamati za Ulinzi kwa Wanawake na Watoto

Posted on: June 27th, 2024

 

Mafunzo hayo ya siku 2 yamefunguliwa na Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Bwana Mozes Chillah kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Toba Nguvila leo Juni 27,2024 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Ilala Boma.

Akifungua mafunzo hayo Ndg Chillah amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa upendo wake kwa watanzania hususani wakazi wa Mkoa huo ambapo upendo wake unajidhihirisha Katika kuhakikisha adhma ya Serikali yake ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na watoto inafanikiwa.

Katibu Tawala Msaidizi Mipango na uratibu amesema ziko jitihada nyingi ambazo zinachukuliwa na Serikali ikiwemo Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ambao umeandaliwa kwa kuunganisha Mipango Kazi tofauti nane iliyokuwa inashughulikia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kutengeneza mpango kazi mmoja.

Aidha MTAKUWWA unalenga kutekeleza adhima ya serikali ya kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambazo ni ukatili wa kingono, kimwili, kihisia na kiuchumi pia Ukatili dhidi ya watoto ni matumizi ya makusudi ya nguvu au vitisho vinavyoweza kusababisha watoto kupata madhara ya kimwili, kiafya na kisaikolojia hivyo kuathiri maendeleo na utu wao.

Hivyo ametoa rai kwa wajumbe wote wa kamati ya Mkoa kufuatilia kwa makini mafunzo hayo ili kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha ujumbe wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na  watoto katika jamii.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wajumbe wengine kama viongozi wa dini, wawakilishi kutoka Jeshi la polisi, wawakilishi wa makundi maalum ya watu wenye ulemavu, Asasi na mashirika yanayojihusisha na kupiga vita vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na watoto ambapo mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 28,2024.


Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila: Miradi 36 yenye Thamani ya Tsh 79,255,160,719.44 Kupitiwa na Mwenge wa Uhuru Dar

    June 01, 2025
  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa