Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametangaza kuanza kwa Kampeni ya Uchangiaji wa Miguu Bandia kwa ajili ya Wananchi 1,000 wenye uhitaji wa Miguu hiyo ili kuwawezesha kutembea na kufanya shughuli zao.
Katika zoezi hilo Wananchi wataweza kutoa Michango yao kwa njia ya Simu, Bank au kufika Ofisi za Mkuu wa Mkoa na kuwasilisha michango yao.
Hatua hii inakuja baada ya wenye uhitaji wa Miguu Bandia*kuwa kubwa tofauti na ile iliyokusudiwa na Mkuu wa Mkoa ya watu 200 ambapo awamu ya kwanza jumla ya watu *650 walichukuliwa vipimo.
Makonda amesema bado uhitaji wa Miguu hiyo ni mkubwa hivyo amewaomba wadau ikiwemo Makampuni, Taasisi na Watu Binafsi kujitokeze kuchangia ili kutimiza dhamira yake ya kuwafanya walemavu kutembea.
Hadi sasa Wadau mbalimbali ikiwemo CCBRT wamechangia Miguu 25 kwaajili ya Miguu ya watu wenye Ugonjwa wa Kisukari, Msanii Mrisho Mpoto miguu mitatu huku Taasisi za MOI, Ajma Othopedics Medical Service wakiunga mkono zoezi hilo.
Baada ya kuona uhitaji ni mkubwa wa Wananchi Kituo cha Utangazaji cha EFM na TV E wameamua kumuunga mkono RC Makonda kwa kuibeba Kampeni hiyo kwa kuhamasisha uchangiaji kupitia vipindi mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa