Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo ametoa msaada wa Generator ya kisasa, Mabati 150 na Mipira 110 kwa Chama cha Mpira wa Kikapu cha Mkoa wa Dar es salaam ili kuwajengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.
Generator hiyo ya kisasa ina uwezo wa KV 35 na haitoi mngurumo wa sauti (silent) ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.
RC MAKONDA amesema anataka kuona Timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa itakayotoa Wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ndani na Nje ya Nchi.
Uamuzi wa RC MAKONDA kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa Kikapu Uwanja wa Taifa na kujionea Uchakavu wa Bati unaosababisha Wachezaji kunyeshewa na Mvua, Ukosefu wa Generator umeme ukikatika na uhaba wa Mipira hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.
Aidha Mhe. PAUL MAKONDA aliahidi kujenga viwanja vitatu vya Mchezo wa Kikapu ambapo tayari ramani imetengenezwa na muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa Viwanja hivyo.
Ili kuendelea kuimarisha Michezo Dar es salaam RC MAKONDA anaunda kamati maalumu ya kushughulikia michezo ya aina zote.
Tayari RC MAKONDA amepata mdau atakaejenga Swimming pool la kisasa Kinondoni kwaajili ya Mchezo wa Kuogelea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam OKARE EMESU amemshukuru RC MAKONDA kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa