-Akutana na kufanya mazungumzo na kamati ya Uongozi wa Wafanyabiashara wa Soko la Karume
- Asema Serikali haina nia yoyote mbaya na wafanyabiashara hao
-Atoa Rai Wafanyabiashara kuendeleza Usalama na Utulivu katika Kipindi cha Siku 7 za Uchunguzi
-Awahakikishia hakuna mwekezaji atapatiwa Soko la Karume
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Januari 18,2022 amefanya kikao na Kamati ya Uongozi wa wafanyabiashara wa Soko la Karume Ofisi kwake Ilala boma - Dar es Salaam.
RC Makalla amesema amekuwa na kikao kizuri cha kuelezana hatima ya Soko lao kufuatia Janga la Moto uliotokea usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 16/01/2022
Mkuu wa Mkoa amewapongeza na kuwashukuru kwa mazungumzo na maelewano baina yao na Serikali akisema Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan inawapenda wafanyabiashara na siku zote dhamira ya Serikali ni kuendelea kuwalea.
" Niseme Serikali haina nia yoyote mbaya na wafanyabiashara wa Soko la Karume niwaombe kuendeleza Usalama na utulivu ndani ya siku 7 za Uchunguzi" Alisema RC Makalla
Aidha RC Makalla ameihakikishia Kamati hiyo Serikali haina mpango wowote wa kumpatia Mwekezaji Soko hilo zaidi Serikali inataka kuona wafanyabiashara wanaendelea kufanya biashara zao maisha yaendelee
RC Makalla amesema kamati itafanya kazi yake kuchunguza mali zilizopotea, chanzo cha Janga hilo la Moto, hatimaye wale wote wailiokuwepo awali wataendelea na biashara zao.
Kwa Upande wa mmoja wa Viongozi wa kamati ya Uongozi ya wafanyabiashara wa Soko la Karume Bi Agusta G Mbata amesema anamshukuru sana RC Makalla kwa Kikao hicho yeye kwa niaba ya wenzake wanaungana na Serikali, wataendelea kupokea maelekezo kwa kuwa wana imani nayo ambapo amesema yeye ni mjane na yuko katika Soko hilo kwa zaidi ya miaka 20 kwa hiyo Kikao cha leo na Mkuu wa Mkoa kimempa faraja kubwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa