Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 1, 2024 akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi Duniani ngazi ya Mkoa ambayo yameadhimishwa katika uwanja wa Uhuru Wilaya ya Temeke.
RC Chalamila akihutubia mamia ya wafanyakazi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho makubwa ya mazingira bora ya wafanyakazi hususani kupandisha mishahara pamoja na kutoa maelekezo maalum ya kuangalia upya kikokotoo kwa watumishi kutokana na kilio cha siku nyingi cha watumishi wa Serikali juu ya jambo hilo. " Mhe Rais Dkt Samia ana dhamira ya dhati ya kufanya maboresho makubwa kwa wafanyakazi kwa masilahi mapana ya Taifa letu" Alisema RC Chalamila.
Vilevile RC Chalamila akijibu Changamoto zinazowakabili wafanyakazi ambazo ziliwasilishwa kwake kupitia risala iliyosomwa na Katibu wa Kanda wa shirikisho la wafanyakazi TUCTA Ndg Meshack Sarota ikiwemo mishahara midogo, ukubwa wa kodi, vitita vya bima ya Afya, Kikokotoo na zinginezo, Mhe RC Chalamila amewahakikishia kutekeleza yale yote yaliyo ndani ya uwezo wake na yale yaliyo nje ya uwezo yatawasilishwa mamlaka husika kwa utekelezaji.
Aidha Mhe Mkuu wa Mkoa amewataka waajiri kutoa zawadi za wafanyakazi bora papohapo ili kuondoa malalamiko ya watumishi hao kutopata zawadi hizo kwa wakati.
Kwa upande wa Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila amewataka watumishi wa umma na binfsi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kuwa wabunifu ili utendaji wao wa kazi uwe na tija pia amesema alishaelekeza kwa waajiri wote katika Mkoa huo kutoa zawadi za wafanyakazi bora papohapo na sio kuahidi.
Mwisho Siku ya wafanyakazi Duniani Kitaifa imefanyika Mkoani Arusha, na mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha sikukuu hiyo katika Uwanja wa uhuru Wilaya ya Temeke
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa