Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wanachama wa Wazohill SACCOS kuendeleza utamaduni wa uendeshaji wa Chama hicho kwa misingi ya Uwazi na Uaminifu ili kukiwezesha chama hicho kukua zaidi ya Sasa.
RC Chalamila amesema hayo akiwa mgeni Rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya Wazo hill SACCOS tangu kuanzishwa kwake, hafla ambayo imefanyika katika Hotel ya Jangwani Sea Bleez Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na wanachama hao RC Chalamila amesema mtaji mkubwa wa mafanikio katika SACCOS yoyote ni uwazi na uaminifu katika uendeshaji wa Chama amekipongeza chama hicho kwa kufikia mafanikio makubwa katika Kipindi chote, huku akiwataka kubadili fedha kuwa rasilimali yenye umiliki kama vile kununua viwanja na vinginevyo vinavyofanana na hivyo.
Aidha Mhe Albert Chalamila alipata wasaa wa kukabidhi vyeti vya pongezi kwa wanachama 6 waliofanya vizuri na hati za Ardhi ambazo ni mafanikio yaliyotokana na Wazohill SACCOSlakini pia ametoa rai kwa wanawake kujiunga na SACCOS kwa kuwa mwanamke ndiye mlezi wa familia
Kwa upande wa Meneja Mtendaji wa Wazohill SACCOS Ndg Samson Kivuyo amesema chama hicho hadi kufikia Juni 22, 2023 kimetimiza miaka 30 huku kukiwa na mafanikio makubwa ikiwemo wanachama kujipatia mikopo mbalimbali ya maendeleo na kuweza kumiliki ardhi tena kwa hati zinazotolewa na wizara ya Ardhi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa