Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 25, 2024 amepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Tsh 38,409,560 kutoka kwa wadau wa maendeleo shirika la JHPIEGO ambao wanashirikiana na Mkoa katika Kuboresha huduma za afya ya uzazi, mtoto na vijana Balehe ( Reproductive Maternal Neonatal Child and Adolescent Health)
Tukio ambalo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Ilala Boma Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila amewashukuru shirika la JHPIEGO kwa kuunga mkono juhudi za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya ambapo ndani ya Kipindi cha miaka 3 ya Rais Dkt Samia Mkoa umeshudia uwekezaji mkubwa Katika sekta ya Afya ya msingi wa takribani Bilioni 52 katika miradi zaidi ya 70 ya ujenzi wa miundombinu na Bilioni 6 katika ununuzi wa vifaa na vifaa tiba mbalimbali.
Aidha RC Chalamila amewataka wataalam kuvitumia na kuvitunza vizuri na kuvifanyia matengezo ya vifaa hivyi ili viweze kudumu muda mrefu.
Mwisho RC Chalamila baada ya kupokea vifaa tiba hivyo kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo amevikabidhi kwa mganga Mkuu wa Mkoa ili viweze kwenda kutumika kwa masilahi mapana ya ustawi wa jamii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa