UTOAJI WA LESENI ZA BIASHARA NA VIBALI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM
Mamlaka za utoaji wa leseni za biashara za kundi ‘B’ zinatoa leseni hizi kwa uwazi kwa kuweka taratibu zinazotakiwa kutimizwa na waombaji na kiasi cha ada wanachotakiwa kulipa kulingana na biashara wanazoomba kwenye tovuti zao na mbao za matangazo ili wanachi wajue kiasi wanachopaswa kulipa na taratibu za kufuata ili kupata leseni. Aidha, malipo yote ya ada za leseni hulipwa kupitia Benki na hivyo kuondoa mwanya wa uvujaji wa mapato ya Serikali. Mwelekeo wa sasa ni kuanza kutoa leseni kwa njia za kieletroniki ili kurahisisha huduma hiyo. Kwa leseni za kundi ‘A’ BRELA wapo katika hatua za mwisho za maandalizi ya utoaji leseni kielertoniki.
Kwa Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ambzo ni mamlaka ya utoaji leseni za kundi ‘B’ zimetoa jumla ya leseni za biashara 60,887 kwa kipindi cha Januari hadi Oktoba 2017 ikilinganishwa na leseni 58,761 kwa kipindi kama hicho mwaka 2016.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa