• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Utalii

UTALII KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM

Mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana katika   uchumi wa Tanzania. Unapatikana katika pwani ya Bahari ya Hindi na una Bandari kubwa katika Afrika mashariki unaoufanya mkoa huu kuwa mashuhuri sana kiuchumu. Una miundombinu ya uhakika ambayo ni barabara nzuri za lami, hoteli zenye hadhi ya kuanzia nyota 1 hadi  5 na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ujulikanao kama (Mwalimu Nyerere International Air Port). Uwepo wa Bandari kubwa na ya kisasa unaufanya Mkoa uweze  kufikika kirahisi kwa kupitia Baharini na Nchikavu kutoka katika kila pembe ya Dunia na kuwa,  kiungo muhimu katika Sekta ya Utalii.

Mkoa wa Dar es Salaam hauko nyuma katika Sekta ya utalii. Mkoa huu unavivutio vingi ambavyo ni muhimu katika kuvutia watalii. Vivutio vya asili vilivyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni Bahari yenye fukwe nzuri, Misitu ya Mikoko na Miyombo, Visiwa, Matumbawe na hifadhi ya wanyama Dar es Salaam zoo.

Dar es Salaam ina uoto wa asili wa aina mbili ambao ni Misitu ya Mikoko yenye ukubwa wa hekta 2760   na Miyombo yenye ukubwa wa hekta 1380.  Misitu ya Mikoko inapatikana katika mwabao wa Bahari ya Hindi na Misitu ya Miyombo inapakika katika maeneo ya uwanda wa juu. Misitu hii imehifadhiwa kwa ajili ya makazi na mazalia ya viumbe wa baharini na nchi kavu na ni kivutio kizuri cha utalii katika mkoa wetu.

Uwepo wa Bahari ya Hindi katika Mkoa huu ni kivutio kizuri sana cha utalii kwa kutoa muonekano unaovutia na kuleta upepo mzuri. Bahari inaweza kutumika kwa kufanya mashindano ya kuendesha boti pamoja na kuogelea. Bahari vilevile ni hifadhi ya samaki wengi wanaovutia. Ufukwe mzuri wa Koko wenye eneo kubwa la kupumzika ni kivutio kizuri cha utalii kwa wenyeji na wageni

Mkoa vilevile una visiwa vikubwa vitatu vilivyo umbali kidogo kutoka katika ufukwe wa Bahari. Visiwa hivyo ni  Mbudya, Bongoyo na Pangavini. Visiwa hivi vina misitu mikubwa ya asili inayopendesha mazingira na ni makazi ya viumbe wa nchi kavu kama vile ndege na nyoka. Vimezungukwa na miamba ya matumbawe (coral reefs) ya rangi mbalimbali na ni mazalia ya samaki.

Mkoa huu unavivutio vingi vya kale ambavyo ni mabaki ya tokea Utawala wa Mwarabu, Mjerumani na Muingereza pamoja na mabaki ya zana na watu wa kale. Mabaki haya yanaonekana kama alama zilizopo ardhini na kwenye majengo.

  • Makumbusho ya Taifa yanayoonesha mabaki ya mafuvu ya binadamu wa kale pamoja na nyayo kutoka katika mapango maarufu ya Olduvai, Hifadhi ya zana za kale za uhunzi pamoja na picha za asili ya makabila mbalimabali.
  • Kijiji cha Makumbusho ni kivutio kizuri cha utalii kinachoonesha tamaduni za makabila yasipungua 100 ya Tanzania. Kinazo nyumba za asili zilizojengwa kwa tope na kuezekwa kwa nyasi na tope. Vivevile kina michoro ya asili, mikeka iliyosukwa kwa mikono na ngoma za asili zinazovutia kucheza.
  • Kunduchi Beach yenye mabwawa makubwa ya kuogelea pamoja na Uwanda mkubwa wa Bahari unaotumika kwa michezo ya kukimbizana kwa pikipiki zamajini ni kivutio kikubwa cha utalii katika Mkoa wetu. Katika hoteli hii kuna maeneo yaliyotengenezwa kwa ajili ya michezo ya watoto na migahawa ya vyakula ambavyo hutia hamasa kutembelea maeneo haya.
  • Vivutio vingine mbalimbali vinavyobeba historia ya ukoloni kuanzia Utawala wa Mwarabu hadi Muingereza ni uwepo wa nyumba za ibada kama vile Msikiti wa Mtoro na Nyamwezi iliyopo kariakoo, Kanisa  (St. Joseph’s , the White Father’s Mission House), 
  • Ikulu Ofisi kuu ya Utawala wa nchi hii yenye usanifu wa kale iliyopambwa na ndege wazuri wasiopatikana eneo lolote Duniani kivutio kizuri cha utalii katika mkoa wetu.
  • Villevile Mkoa unatambulika kwa kuwa na hoteli zenye hadhi ya nyota tano ambazo zinatoa uhakika wa malazi salama kwa watalii.

Ushirikiano na Miji mingine ya Utalii Duniani ni jambo muhimu sana, tunaweza kuibadilisha Dar es Salaam kuwa Jiji kuu la Utalii Duniani na kuliongezea Taifa kipato. Si hivyo tu bali uchumi wa watu utabadilika na kupunguza umasikini. Kwa kuzingatia kwamba Serikali yetu inasisitiza mabadiliko katika kuboresha uchumi wa viwanda ili kuondoa umasikini na kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa