• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Management,Monitoring and Inspection
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Industry, Trade and Investiment
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Government Communication Unit
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Muongozo wa Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Biashara

Utangulizi

Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa asilimia 62 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam lina jumla ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 hadi 64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara na ajira viwandani.


AINA ZA BIASHARA

Kuna aina tatu za biashara zinazotambuliwa

  1. Biashara ya jumla
  2. Biashara ya rejareja
  3. Biashara ya Kimataifa: - Uagizaji bidhaa toka nje (Import) na Uuzaji bidhaa kwenda nje (Export)


(a) BIASHARA YA JUMLA

Katika Jiji la Dar es Salaam kuna bidhaa za aina mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango kikubwa na kupelekwa nje ya Mkoa. Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.

(b) BIASHARA YA REJAREJA

Hii ni biashara inayofanywa kwa kuuza bidhaa zilizonunuliwa jumla na kuuzwa kidogo kidogo kwa mlaji wa mwisho. Bidhaa hizi ni za aina nyingi sana zikiwemo vyakula, vifaa vya ujenzi, mavazi na bidhaa zingine zote za matumizi mbalimbali. Biashara hizi hupatikana katika masoko, maduka na maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili hiyo.

(c) BIASHARA YA KIMATAIFA

Biashara hii inafanyika katika Nchi yetu na nchi za nje ambapo kuna aina: Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import) na Uuzaji bidhaa kwenda Nchi za nje (Export)

  • Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import)

Kuna makampuni mbalimbali yanayoagiza bidhaa toka nje ya nchi na kuzisambaza mikoani. Bidhaa zinazoagiza nje ni pamoja na nguo, vifaa vya ujenzi kwa mfano mabati, magari, vipuri vya magari, vipuri vya mashine, baiskeli, pikipiki.

  • Uuzaji wa bidhaa Nchi za nje (Export)

Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi ni pamoja na mazao ya kilimo kwa mfano kahawa, katani, tumbaku, majani ya chai, korosho, karanga na maua. Uagizaji wa bidhaa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje unasimamiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE).

MADUKA MAKUBWA

Kuna maduka makubwa yanayouza bidhaa jumla na rejareja na kuagiza bidhaa toka nje. Maduka hayo ni:-

  • Nakumatt
  • Shoppers Plaza
  • Quality Centre
  • Mlimani City
  • Imalaseko
  • Hidary Plaza
  • J. Mall n.k.

MASOKO

Katika Jiji la Dar es Salaam idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa haraka kutokana na vivutio vya shughuli za biashara na viwanda. Wakazi hawa hupata mahitaji yao kwa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye Masoko. Kuna jumla ya masoko 61 yanayosimamiwa na Halmashauri za Manispaa na moja linasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

  • Temeke 17
  • Ilala 24
  • Kinondoni 19
  • Halmashauri ya Jiji 1 (Machinga Complex)

Kati ya Masoko ambayo idadi yake imeoneshwa hapo juu, masoko makubwa ni Kariakoo, Tegeta, Buguruni, Temeke Sterio, Kawe, Ilala, Tazara (Veteririnary) na Feri. Serikali imejenga soko kubwa (Machinga Complex) linaloweza kuchukua wafanyabiashara/wajasiriamali 6,000 lakini jengo hili halijatumika/halijachukua wajasiriamali wengi kama ilivyotarajiwa.


HUDUMA ZA BIASHARA

Kuna huduma za biashara zinazotolewa na Taasisi mbalimbali.

Benki

Kuna Benki za Biashara zipatazo 34 kati ya hizo ni:

  • CRDB
  • National Bank of Commerce
  • Standard Chartered
  • National Microfinance
  • Bank of Baroda
  • Kenya Commercial Bank
  • International Commercial Bank
  • FBME Bank
  • Equity Bank (Tanzania)

Taasisi za Fedha

Kuna taasisi zinazotoa huduma za fedha katika Jiji la Dar es Salaam zikiwa ni pamoja na zifuatazo:-

  • Efatha
  • Finca Tanzania Ltd
  • Maendeleo Bank
  • Anzania Investment Bank
  • Tanzania Mongange Refinance Bank
  • Twiga Barcorp Ltd
  • Uchumi Commercial Bank Ltd
  • Convenant Bank for Women
  • Exim Bank

Maduka ya fedha (Bureau de change)

Maduka hayo huuza fedha za ndani na za kigeni. Maduka hayo ni mengi na yamesambaa katika maeneo mengi ya Jiji.

Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania


Maduka ya Madawa

Kuna maduka makubwa ya madawa yanayotoa huduma ya kuuza madawa kwa jumla na rejareja.

  • Salama Phamaceticals Ltd
  • JB Phamacy etc.

VIWANDA

Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu katika uchumi wa Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya aina mbalimbali kufuatana na bidhaa zinazozalishwa.

(a) Viwanda vya nguo viko 36 kati ya hivyo ni:

  • Karibu Textile Mills Ltd
  • Tanzania China Friendship Textile
  • Nida Textile Mills (t) Ltd
  • 21 st Century Textile
  • Tanzania Uniform and Clothing Corporation Ltd
  • Quality Textile
  • Tanzania clothing Co. Ltd
  • Textile Manufacturers Association
  • Textile Manufacturers (T) Ltd
  • Tex Age Tanzania Ltd
  • Traditional Textiles (T)
  • Tanganyika Textiles Industries Ltd
  • Tanzania Knitwear Co. Ltd
  • Tradenet International Ltd
  • Varieties Textile Merchant
  • Viraj Textile
  •  Afri Care
  • Blanket Textiles Manufacturers Ltd
  • Blanket & Textile Ltd
  • Congolin & Co. Ltd
  • Fomoka Trading and Industry Co. Ltd
  • J.V. Textile & Cryarments Ltd
  • K.H. Khimji & Sons
  • Kilimanjaro Textile Corporation
  • Fashion Fabric Textile etc

(b) Viwanda vya Kusindika Vyakula

  • Dyestuffs, Chemicals & Food Colors
  • Msk Solutions
  • Olan Tanzania
  • Power Food Industries
  • Bakhresa Group
  • Noble Azania n.k.
  • Fishmeal and Animal Protein

(c) Viwanda vya Vinywaji

  • Tanzania Breweries Ltd
  • Serengeti Breweries Ltd
  • Cocacola Kwanza Ltd
  • SBC (Pepsicola)
  • Chibuku
  • Tanzania Distritaries

(d) Viwanda vya Kutengeneza Kemikali

  • Quality Plastics Ltd
  • Polypet Industries
  • Mansoor Daya Chemicals Ltd
  • Plasco Ltd
  • Twiga Chemical Industries (T) Ltd
  • Abcom Chemicals Ltd
  • Afro Chemicals Ltd
  • Bio-Chemicals Laboratory Supplies Ltd

VIWANDA VIDOGO

Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO) linatoa mafunzo kwa wajasiriamali na kuanzisha viwanda vidogo vidogo kama vile:-

  • Utengenezaji wa samani mfano Keko Furniture Works
  • Utengenezaji wa vyakul vya mifugo (Temeke Growers Meal)
  • Aluminium Scrap
  • Mkono Arts & Crafts
  • Confectionary & Beverages
  • Wine Products
  • Gifts, Crafts & Home Decorations
  • Poultry, Farming Equipments


EPZA (Export Processing Zone Authority)

Hii ni Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya Nje. Inashughulikia maeneo yaliyotolewa na kuendelezwa kwa ajili ya kuvutia na kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje. Maeneo haya huzalisha bidhaa kwa ajili ya kuuza nje tu (exports). Maeneo ya EPZA kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni:

  • Benjamin Mkapa Export Processing Zone
  • Millennium Business Park (Ubungo)
  • Hifadhi Economic Processing Zone (Ubungo)
  • Manzava Fabries Co. Ltd
  • Kurasini Export Processing Zone. Hili eneo bado linajengwa na litahusika sana na mazao ya kilimo.  


VITEGA UCHUMI VIKUBWA VYA AINA YA PEKEE

Mkoa wa Dar es Salaam una vitega uchumi vikubwa vya aina ya pekee kwa ukubwa na huongeza mapato Kitaifa. Vitege uchumi hivyo ni:-

  • Bandari ya Dar es Salaam
  • Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu J.K. Nyerere
  • Uwanja wa Taifa
  • Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere
  • Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU (MOCK) MKOA WA DARASA LA SABA - 2024 July 05, 2024
  • KARIBU MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI MHE HARRIS KAMALA March 29, 2023
  • KARIBU MWENGE WA UHURU 2023 May 24, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Chalamila Ataka Machinga Kariakoo Kufungua Njia

    May 28, 2025
  • CHALAMILA SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI KAZI YA UUGUZI

    May 23, 2025
  • Mchengerwa: Maafisa Habari Hakikisheni Wanachi Wanapata Habari Sahihi

    May 23, 2025
  • RC Chalamila Akabidhi Magari Mapya Mawili (2)-DSM

    May 20, 2025
  • Tazama zote

Video

RC Chalamila Azindua Wiki ya Sheria DSM
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa