• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Mkoa  wa Dar es Salaam

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es Salaam

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Muundo wa Kiutawala
  • Utawala
    • Seksheni
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maji
      • Elimu
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Ilala
    • Kinondoni
    • Temeke
    • Ubungo
    • Kigamboni
  • Halmashauri
    • Jiji
    • Kinondoni MC
    • Temeke MC
    • Ubungo MC
    • Kigamboni MC
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Biashara
    • Utalii
  • Huduma Zetu
    • Maji
    • Afya
    • Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu Mbalimbali
    • Taarifa Mbalimbali
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
      • Bofya hapa
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawatangazia wananchi wenye Matatizo ya macho kufika kwenye kambi ya macho iliyopo Mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili kupatiwa vipimo,matibabu na miwani bure.

05 October 2017


 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RC MAKONDA KUSAIDIA WAGONJWA 1,000 KUPATIWA MATIBABU YA MACHO NA MIWANI BURE

Mwendelezo wa zoezi la Upimaji wa Afya Bure kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye Matatizo ya Macho linaendelea na sasa ni Huduma ya Matibabu ya Macho kwa Wananchi waliobainika kuwa na Matatizo ya Macho kwenye Kampeni ya RC Makonda ya Upimaji wa Afya Bure.

 Zoezi hilo ni kufuatia ahadi iliyotolewa na Jumuiya ya Waislamu wa Dhehebu la Khoja Shia Ithnasheri Jamaat K.S.I.J iliyojitolea kumuunga Mkono RC Makonda kwa kujitolea Matibabu ya wagonjwa watakaobainika kuwa na matatizo ya Macho na Mtoto wa jicho kwenye Kampeni ya Upimaji Afya Bure iliyofanyika Mnazi mmoja

Zoezi hilo linasimamiwa na Madaktari bingwa wa Macho kutoka Hospital ya Muhimbili, Hindumandal na Ebrahim Haji.

Kutokana na uhitaji kuwa mkubwa Mhe. Makonda ameomba Taasisi hiyo kupima na kufanya matibabu kwa wagonjwa 1,000 badala ya 500 iliyoahidi ambapo wameridhia ombi hilo.

Amesema kuwa kwa kawaida Garama za upasuaji wa Macho ni kati ya Shillingi 900,000 hadi 1,000,000 pamoja na miwani hivyo kwa watu 1,000 ni sawa na Kiasi cha Shillingi Billioni Moja lakini kupitia wadau wagonjwa hao watapatiwa matibabu na Miwani Bure ili waone Matunda ya Serikali ya awamu ya Tano kupitia RC Makonda

RC Makonda anawahimiza wananchi wenye Matatizo ya Macho kufika kwenye kambi ya matibabu ya Macho iliyopo mtaa wa Hindragand Posta kila Jumamosi na Jumapili kwa kipindi cha Miezi Miwili ili wapatiwe Vipimo, Matibabu na Miwani Bure kwa wenye uhitaji.

Ameshukuru wadau hao kwa kumuunga mkono na kueleza kuwa lengo lake ni kuwawezesha wananchi wasioweza kumudu gharama za matibabu kupata huduma.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Habari na Uhusiano

OFISI YA MKUU WA MKOA

 DAR ES SALAAM

05/10/2017

Matangazo

  • RATIBA YA KAZI YA MHE. RC MAKALLA KUANZIA 20 - 26 APRIL,2022 April 20, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Utamilifu (Mock) Mkoa wa Darasa la Saba - 2021 July 30, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA BEI ELEKEZI YA MBOLEA March 30, 2022
  • Matokeo ya Mtihani wa Mock Mkoa Darasa la Saba - 2020 September 02, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Dar es Salaam Yaadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani

    May 24, 2022
  • DC Ilala Ataka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kuchukua Hatua kwa Wanaokaidi Maelekezo Wanayoyatoa

    May 19, 2022
  • "Dar es Salaam Mmefanya Vizuri Oparesheni ya Anwani za Makazi na Postikodi" Waziri Nape

    May 18, 2022
  • RC Makalla Apokea Kero zaJumuiya ya Wafanyabiashara Dar es Salaam.

    May 16, 2022
  • Tazama zote

Video

Maelekezo ya RC Makalla juu ya Mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko DSM.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
  • Wilaya ya Ilala
  • Wilaya ya Kinondoni
  • Wilaya ya Temeke
  • Wilaya ya Ubungo
  • Wilaya ya Kigamboni

Tovuti Muhimu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofis ya Rais-Utumishi
  • Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

    Anuani ya Posta: S.L.P. 5429

    Simu ya mezani: +255 22 2203158

    Simu ya mkononi: +255 22 2203156

    Barua pepe: ras@dsm.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa