TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DAR ES SALAAM KUZINDUA SOKO LA MADINI NA VITO KESHO JUMATANO JULAI 17.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda anawaalika Wadau Wote wa Madini na Wananchi kwenye Uzinduzi wa Soko la Madini na Vito unaotarajiwa kufanyika kesho Jumatano ya Julai 17 kwenye Jengo la NHC jirani na Makao Makuu ya TTCL.
Uzinduzi wa Soko la madini na vito ni hatua ya utekelezaji wa Agizo alilotoa Rais Dkt. John Magufuli kwa kila mkoa kuhakikisha unakuwa na sehemu maalumu ya Soko la Madini na Vito.
Uzinduzi wa Soko hilo utahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Madini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda, makatibu wakuu, wakuu wa wilaya, makatibu tawala na watendaji wengine.
DAR ES SALAAM TUNATEKELEZA KWA VITENDO.
Imetolewa na:-
Kitengo cha Habari na Uhusiano
OFISI YA MKUU WA MKOA
DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa