JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
USHIRIKA:
 
Ushirika [ Nyumbani ]
 
 
 
 

Vyama vya Ushirika

 
 
 

Vyama vya Ushirika huanzishwa na kuandikishwa kwa kuzingatia Sheria ya Ushirika ya Mwaka 2003. Mkoa una jumla ya Vyama vya Ushirika 879 vilivyoandikishwa vikiwemo Vyama vikuu vya Ushirika (Unions) vitatu (3) ambavyo ni Chama Kikuu cha Ushirika cha Mazao (DARECU), Chama Kikuu cha Viwanda (TICU) na Chama Kikuu cha Akiba na Mikopo (SCCULT) Ltd. Pia kuna vyama vitano (5) vya Ubia (Joint Venture Enterprises).

 
  • DARECU ni Chama Kikuu cha Ushirika cha mazao ambacho kazi yake ni kununua mazao ya wakulima na kusambaza pembejeo kwa kushirikiana na Vyama vya Msingi 23 ambavyo ndio wanachama wa Chama hiki.
 
  • SCCULT (1992) LTD ni muungano wa Vyama vya Akiba na Mikopo Tanzania, kazi yake ni kutoa ushauri na kuvisaidia Vyama vya Msingi vya Akiba na Mikopo katika kupata mitaji na mafunzo.

 
  • Vyama vya Ubia (Joint Venture Enterprises) ni Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Kibiashara katika maeneo ya Masoko. Kazi ya vyama hivi vya Ubia ni kuwasaidia wafanyabishara kupata elimu ya biashara na mitaji
  • SACCOS ni Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo ambavyo vinatoa huduma ya mikopo kwa Wanachama katika kupata mitaji ya kuendeshea biashara mbalimbali na kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi.

 
 
Hadi kufikia mwezi Desemba 2013, Mkoa ulikuwa na jumla ya Vyama vya Ushirika vya Msingi 871 vilivyo- andikishwa
Ki-Sheria; ambapo Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) ni 662, Vyama vya mazao (korosho) 23, na Vyama 186 vya aina nyingine kama vile ujenzi wa Nyumba, Viwanda, Biashara, Usafiri na Uvuvi.
 
 
 
 
 
 
 

Hali ya Vyama (Wanachama, Hisa, Akiba na Mikopo)Wanachama :

 

Vyama vya Ushirika hapa Mkoani vina jumla ya wanachama 208,233 hadi mwezi Desemba 2013, kati yao, SACCOS zina wanachama 193,930.

 
 
Hisa, Akiba na Mikopo

 

Wanachama katika SACCOS wamenunua Hisa zenye thamani ya Shilingi Bilioni 10.8, pia wameweka Akiba na Amana zenye thamani ya Shilingi Bilioni 108.67 hadi Desemba 2013. Mikopo iliyotolewa kwa wanachama hao hadi Desemba, 2013 ni ya thamani ya Shilingi Bilioni 226.5

 

Ukaguzi wa Mahesabu wa Usimamizi wa Vyama

 

Mkoa kupitia Maafisa Ushirika wake umeweza kufanya ukaguzi na usimamizi wa Vyama na kutoa ripoti kwa Wanachama wake kwa Vyama 352 kati ya Vyama vilivyo hai 652 hadi Desemba 2013 sawa na asilimia 54.% ya Vyama ambavyo ni hai.

 

 

Moja ya jengo la chama cha ushirika -WANAMA SACCOS

 

 

 
     
     
 
         
 
Ushirika [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213