JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
USAFIRI NA MAWASILIANO JIJINI
 
Usafiri & Mawasiliano [ Nyumbani ]
 
 
 
 
USAFIRI
 

Usafiri wa Daladala Mkoani Dar es Salaam:

 
 

Daladala ndio usafiri mkuu wa umma unaotumiwa na wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam. Pia kipo kituo kikubwa cha mabasi yanayotoka na kuingia Dar es Salaam kutoka mikoani na nchi jirani kilichopo Ubungo (Ubungo Bus Terminal)

 
 
Usafiri wa Anga:
 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere upo upande wa magharibi wa Jiji la Dar es Salaam katika Kata ya Ukonga. Uwanja huu hutoa huduma zote za usafiri na usafirishaji wa abiria na Mizigo kitaifa na kimataifa
 

Usafiri wa Majini:

 
 

Bandari ya Dar es Salaam ambayo ipo chini ya Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), inatoa huduma ya usafiri ndani na nje ya nchi.

 
 

 

Usafiri wa Reli:

Makao makuu ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) na Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) yapo jiji Dar es Salaam . Mashirika haya hutoa huduma ya usafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani na nchi jirani za Zambia , DRC, Rwanda , Burundi na Uganda .

 
 
 
 
 

kivuko cha Magogoni- Mkoani Dar es Salaam

 
 
MAWASILIANO:
 

Simu:

 

Makampuni sita(6) ya simu: VODACOM, AIRTEL, TIGO, ZANTEL SASATEL na TTCL yanatoa huduma katika Jiji la Dar es Salam

 
 
Posta:
 

Makao makuu ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) yapo katikati ya Jiji Dar es Salaam katika eneo maarufu linalojulikana kama 'POSTA', Aidha katika Halmashauri za Manispaa zote tatu zipo 0fisi za Posta

 
Fax(Nukushi) na Internet:

 

Huduma za fax na Internet ziemeenea katika kila kona ya Jiji la Dar es Salaam . Huduma hii inafanyika kibiashara zaidi na Makampuni pamoja na watu binafsi kwa bei ya Ushindani katika soko.

Usafiri wa reli
   
     
 
         
 
Usafiri & Mawasiliano [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213