JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
SERIKALI ZA MITAA
 
Serikali za Mitaa [ Nyumbani ]
 
 
 
Mkoa wa Dar es Salaam una Halmashauri za Manispaa tano (5) ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke, Ubungo, Kigamboni na Halmashauri ya Jiji.
 

Halmashauri za Manispaa pamoja na Halmashauri ya Jiji zinaongozwa na Wastahiki Mameya ambao ni Wenyeviti wa Halmashauri, kwa kushirikiana na Wakurugenzi ambao ni Watendaji wakuu wa Halmashauri husika .

 
 
 
Halmashauri za Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Halmashauri ya Jiji hutoa huduma za Kiuchumi zikiwepo kilimo, mifugo, misitu, Uvuvi, miuondombinu, huduma za jamii kama afya, maji, elimu, maeneo ya burudani, mazishi, mipango miji, kutunza mazingira, ustawi wa jamii, ushirika na mambo mengine yanayoihusu jamii na Taifa kwa ujumla
 
 

Utawala bora ni suala linalotekelezwa na Halmashauri zote katika nyanja za:

•  Demokrasia

•  Ushirikishwaji

•  Utawala wa sheria

•  Uadilifu wa viongozi na wafanyakazi wa Serikali za mitaa

•  Uwazi na Uwajibikaji

•  Ufanisi katika utendaji kazi

•  Mchakato wa kijinsia

•  Upangaji mipango

•  Ujuzi wa upangaji Mipango kwa kutumia Rasilimali zilizopo

•  Utekelezaji wa Mipango.

 
 
 
 
 
 
MAJUKUMU YA SERIKALI ZA MITAA.
 

Halmashauri za Manispaa zimeanzishwa chini ya sheria za Mamlaka za Miji (Local Government Urban Authorities Act. 1982).
Majukumu makuu ya Serikali za Mitaa yaliyofafanuliwa na sheria hiyo ni kama ifuatavyo:-

 • Kusimamia na kudumisha amani ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka yake.
 • Kuhamasisha/kuendeleza na kuwapatia huduma bora za kijamii na kiuchumi wananchi walio katika eneo la mipaka ya Halmashauri.
 • Kusimamia sera za maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo yao.
 • Kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kuendeleza mazingira.
 • Kusimamia utawala, fedha, mambo yote ya uendeshaji katika ngazi mbalimbali zilizo ndani ya mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa/Jiji.
 • Kusimamia na kuhakikisha demokrasia inadumishwa katika jamii.
 • Kukusanya mapato yatakayowezesha Mamlaka ya Serikali ya Mtaa kuendesha shughuli zake pamoja na kutoa taarifa za matumizi kupitia kamati mbalimbali.
 • Kutoa huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
 • Kuzingatia na kutambua masuala mtambuka kama vile Jinsia.
 • Kuendeleza na kusimamia kanuni za biashara, viwanda, kilimo n.k.
 • Kusimamia na kuendeleza huduma za Afya, Elimu, Maji, Utamaduni na masuala ya burudani katika jamii.
 • Kubuni mikakati ya kupambana na umaskini pamoja na mbinu za kusaidia kuboresha maisha ya vijana, wazee, walemavu n.k.
 
 
 
 
 
 
 
     
     
         
 
Serikali za Mitaa [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213