JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MAZINGIRA
 
[ Maliasili ] Mazingira [ Nyumbani ]
 
 
 
 
Utangulizi

 

Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji. Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu namazingira.
 

Juhudi za Serikali katika kutunza Mazingira

Kuzuia uchimbaji haramu wa kokoto, mchanga na vifusi

Katika kudhibiti uharibifu wa ardhi kutokana na uchimbaji holela wa kokoto, vifusi na mchaga, Uongozi wa Mkoa ulitoa tamko linalozuia shughuli hizo katika maeneo ya yote ya Jiji la Dar es Salaam. Maeneo ambayo tayari yameathirika sana na uchimbaji huo ni pamoja na mabonde ya mito (Mpiji, Majani ya Chai na Msimbazi) na maeneo ya Pugu Golani na Kunduchi Beach.  

Kutoa elimu ya usafi na utunzaji wa mazingira
Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Dar es Salaam zinawajibika kusimamia usafi wa mazingira. Wajibu huo unafanyika kwa kushirikisha ngazi zote za serikali na wadau mbalimbali kama vile sekta binafsi na wakazi katika ngazi ya kaya.

Usimamizi wa sheria za utunzaji wa mazingira
Mamlaka za Serikali za Mtaa katika Mkoa wa Dar es Salaam zina sheria zinazohusu utunzaji, uhifadhi na uendelevu wa mazingira. Katika kusimamia sheria hizo, shughuli zinazofanyika katika maeneo yasiyoruhusiwa huondolewa. Changamoto iliyopo ni uhamiaji mkubwa wa watu kuja Jijini kufanya shughuli mbalimbali, hususan za kibiashara; wakiwa na imani kwamba kuna fursa ya kufanikiwa wakifanya shughuli hizo Jijini Dar es Salaam.

 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
Eneo la Pwani ya Dar es Salaam
 

 

Aidha kila mwaka Mkoa unashiriki katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambapo utekelezaji wa maadhimisho hayo huanza tarehe 01 Juni, na kila Halmashauri kushiriki kwa kufanya shughuli mbalimbali za usafi na uhifadhi mazingira katika maeneo mbalimbali.
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 

 

 

 

 

     
     
 
         
 
[ Maliasili ] Mazingira [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213