JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MALIASILI
 
Maliasili [ Mazingira ] [ Nyumbani ]
 
 
 
Utangulizi
 

Eneo la Misitu:
Mkoa wa Dar es salaam una ukubwa wa eneo lenye kilometa za mraba 1,397 ambapo eneo lenye misitu ni kilometa za mraba 41.4.

Uoto wa asili katika Misitu iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam

 
 
 

Uoto wa asili uliopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni misitu ya mikoko na miombo. Misitu ya mikoko inapatikana katika mwambao wa Bahari ya Hindi, ina ukubwa wa kilometa za mraba 27.6 na ndiyo yenye uoto mkubwa wa asili katika Mkoa wa Dar es salaam. Misitu ya Miombo haina uoto mkubwa wa asili, inakadiriwa kuwa na ukubwa wa kilometa za mraba 13.8 yenye miti jamiii ya Acasia, Mipingo, Mninga, Mikongo, Mikoche na Migude.

Faida za misitu


Mandhari nzuri
Misitu ni pambo inayotoa mandhari nzuri kwa jamii inayozunguka hata kuvutia wageni toka nje kufanya utalii. Mkoa wa Dar es salaam una mandhari nzuri inayotokana na Bahari ya Hindi iliyopambwa na msitu wa mikoko, inatoa eneo zuri la kupumzikia kwa wenyeji hata wageni kutoka katika nchi mbalimbali duniani. Sambamba na hilo serikali, watu binafsi, na taasisi zisizo za kiserikali zimekuwa mstari wa mbele katika kutengeneza bustani za miti na maua kwa ajili ya mapambo na biashara. Bustani hizi zilizopo katika nyumba za makazi, pembezoni mwa barabara, ofisi na maeneo mbalimbali ya biashara na shughuli za kijamii zinatoa mandhari nzuri inayovutia pamoja na vivuli kwa ajili ya kupumzikia.

Ajira kwa jamii
Mazao ya misitu kama vile mbao, kuni, mkaa, ukindu, milala na asali vimekuwa vikitoa ajira kubwa kwa jamii hasa vijana. Biashara ya miche ya miti ya aina mbalimbali ni maarufu katika maeneo mbalimbali ya Jiji.

Ufugaji wa nyuki
Shughuli za ufugaji wa nyuki zinaendeshwa na vikundi mbalimbali na watu binafsi.

 
upandaji miti
Juhudi mbalimbali zinafanywa na Serikali, taasisi mbali mbali na watu binafsi katika upandaji wa miti. Miti hupandwa katika maeneo ya fukwe, misituni, pembezoni mwa barabara, maeneo ya ofisi na katika maeneo ya makazi. Kila mwaka Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Halmashauri zake hushiriki katika Kampeni ya Upandaji Miti Kitaifa.
 
Uhifadhi za Misitu

 

Miti ya Mikoko kama inayoonekana katika eneo la fukwe - Mtoni kijichi
 

 

 

 

 

 
 
 
     
Aidha kampeni ya upandaji miti ijulikanayo kama 'MTI WANGU' iliyoasisiwa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda, ilizinduliwa rasmi tarehe 01 Oktoba, 2016 katika barabara ya Kilwa, Kampeni hii ni ya miaka minne, yenye lengo la kupanda miti 4,500,000 (milioni nne na laki tano) katika Mkoa wa Dar es Salaam.
   
     
     
 
         
 
Maliasili [ Mazingira ] [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213