JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
YANAYOTUHUSU
 
Kutuhusu [ Contacts ] [ Nyumbani ]
 
 
Mipaka na Eneo
 

Mkoa wa Dar es Salaam unapakana/umezungukwa na Mkoa wa Pwani kwa pande za Kaskazini, Magharibi na Kusini Magharibi. Bahari ya Hindi ndiyo mpaka wa Mkoa kwa upande wa Mashariki na Kusini Mashariki, ambapo una ufukwe wenye urefu wa km. 124. Eneo la Mkoa ni Kilomita za mraba 1,397. Kati ya eneo hilo kilomita za mraba 452 ndizo zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Mji na 673 ni eneo linalofaa kwa kilimo na ufugaji. Aidha, kilomita za mraba 272 ni eneo la maji katika Bahari ya Hindi.

 
 
 

Hali ya Hewa:

 

Hali ya hewa ya Mkoa wa Dar es Salaam ni ya joto la wastani wa nyuzi joto 25 28 o C kati ya miezi ya Juni hadi Agosti na nyuzi joto 29 33 0 C kwa miezi iliyosalia. Mkoa hupata mvua za wastani wa mm 800- 1000 katika misimu miwili ya vuli ambayo ni miezi ya Oktoba Desemba na Masika ambayo huanza miezi ya Machi Mei.

 

 

Idadi ya Watu:

 
 

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 Mkoa wa Dar es Salaam una idadi ya wakazi 4,364,541, ambapo kati yao wanaume ni 2,125,786 na wanawake ni 2,238,755.

 
Sehemu ya Utawala
Mkoa wa Dar es Salaam ulianzishwa mwaka 1973. Mkoa una jumla ya Wilaya tatu ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke, Tarafa 10, Kata 90 na Mitaa 453 Pia una majimbo ya uchaguzi 8. Mkoa umegawanyika katika Mamlaka 4 za Serikali za Mitaa ambazo ni Halmashauri ya Jiji, Halmashauri za Manispaa 3 za Ilala, Kinondoni na Temeke zilizoanza rasmi mwaka 2000.
 
 
 
 
 
Ramani ya Mkoa wa Dar es Salaam
 
 
 
Mgawanyiko wa Majimbo ya Uchaguzi, Tarafa, Kata na Mitaa ni kama ifuatavyo
 
Wilaya Majimbo Tarafa Kata Mitaa

Ilala

3

3

26

102

Kinondoni

3

4

34

171

Temeke

2

3

30

180

Total

8

10

90

453

 
Ulinzi na Usalama

Kiusalama mkoa unaongozwa na Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa upande wa Polisi, Usalama wa Taifa na PCCB. Una Makamanda 3 wa Polisi wenye hadhi ya ngazi ya Mkoa na Wakuu wa Usalama wa Taifa 3 wenye hadhi sawa ambao kiutendaji wapo katika ngazi ya Wilaya. Aidha, Vyombo vya ulinzi katika Mkoa ni pamoja na Uhamiaji, Magereza na Mgambo.

 

 

     
 
         
Kutuhusu [ Contacts ] [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-022-2203213