JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MIFUGO
 
[ Kilimo ] Mifugo [ Nyumbani ]
 
 
 
Utangulizi
 

Katika Mkoa wa Dar es Salaam upo ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali kwa wanyama wakubwa na wadogo, kwa ajili ya chakula , biashara, wanyamakazi na wanyama rafiki (pets). Shughuli za ufugaji zinafanyika kwa idadi maalum kutegemeana na aina ya mifugo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Aidha ufugaji huu unasaidia kwa kiwango kizuri kutoa ajira kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, ufugaji huu unatakiwa uwe endelevu na wenye kuzingatia kanuni za ufugaji bora.

 
 
 

Huduma za ugani:

 

Huduma za ugani hutolewa na wataalam wa mifugo wa Serikali wa Halmashauri za Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na sekta binafsi katika klinik na vituo vya mifugo.

 
 
Indigenous cattle keeping are not prominent in the region. These supply the draught animals and others are reared for slaughtering and milk. In some periods few cattle are brought in from other regions for fattening and then slaughtered or exported to Arabian countries and Comoro. The region slaughters an average of 800-1000 cattle daily
 
 

Huduma zinazotolewa na Wataalamu wa Mifugo wa Serikali:-

  1. Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
  2. Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
  3. Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba
  4. Ukaguzi wa nyama na ngozi
  5. Kutoa vibali vya kusafirisha mifugo
  6. kutoa vibali kwa watu walioumwa na mbwa/wanyama kuweza kupata chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha mbwa katika hospitali za binadamu.
 

Huduma zinazotolewa na wataalam wa sekta binafsi:

 

1.  Kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo
2.  Kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora
3. Uhamilishaji (A.I.) na kupima mimba

 

 

 

 
 

Aina ya mifugo katika Mkoa wa Dar es Salaam

 

Mkoa wa Dar es Salaam una aina mbalimbali za mifugo na idadi yake ni kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo:

 
 

Aina ya mifugo

Idadi

Ng'ombe wa Kisasa

36,806

Ng'ombe wa Kienyeji

10,451

Mbuzi

31,558

Kondoo

7,427

Nguruwe

43,022

Kuku

6,842,734

 

Mifugo mingine iliyopo katika Mkoa wa Dar es Salaam ni bata 27,640 (bata maji 26,077, bata bukini 45 na bata mzinga 1,463) kanga 4,469 kwale 1,520 sungura 1,118 simbilisi 162 mbwa 14,504, punda 128 farasi 18 ngamia 105 na paka wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 2,524.

 
Miundombinu ya Mifugo
 

Maduka/ Maeneo ambayo pembejeo za mifugo (vyakula vya mifugo, madawa, chanjo) pamoja na vituo vya huduma kwa mifugo ambayo ni 13, yapo katika maeneombalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.

 
Viwanda vya usindikaji wa mazao ya mifugo ambavyo idadi yake ni: Maziwa 6, ngozi 4, nyama 3, kuku wazima 2 na vyakula vya mifugo visiopungua 45
 
Miundombinu mingine ni mnada wa upili (secondary market), majosho, malambo, mabirika, vibanio, mabanda ya ngozi, machinjio, machinjio (slabs) (kwa ajili ya ng'ombe,nguruwe,kuku na ndege wengine.) idadi ni kama inavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo
 

Aina ya mifugo

Idadi

Machinjio za ng'ombe, mbuzi na kondoo

7

Machinjio za nguruwe

19

Machinjio za kuku

16

 

Katika mnada wa upili wa Pugu tunapokea wastani wa ng'ombe 800-1000 kwa siku , mbuzi 200-400 na kondoo 100-250 kwa siku

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

     
     
 
         
 
[ Kilimo ] Mifugo [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2860081/2863716, FAX: 022-2863716