JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
KAZI
 
Kazi [ Nyumbani ] au
 
     
     
    Kwa mujibu wa sheria, yaani Sheria ya Taasisi za Kazi ya Mwaka 2004, utatuzi wa Migogoro ya kazi hufanywa na Tume
ya Usuluhishi wa Migogoro na Uamuzi ambayo ni tume huru .
     
    Pamoja na utatuzi wa Migogoro ya kazi kufanywa na Tume huru ya Usuluhishi bado ushauri hutolewa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa wadau wenye matatizo mbalimbali yanayohusu kazi . Aidha Mkoa husimamia na kutoa ushauri kama utakavyohitajika kuhusu shughuli za ukaguzi sehemu za kazi, na usimamizi wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi wanaoumia kazini .
     
    Kufuatia kuanza kutumika kwa sheria mpya za kazi yaani, Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini ya Mwaka 2004 na Sheria
ya Taasisi za Kazi ya Mwaka 2004, Usimamizi wa sheria inayohusu migogoro hufanywa na Tume ya Usuluhishi wa Migogoro
na Uamuzi; sheria zinazohusu fidia kwa wafanyakazi wanaoumia kazini, masuala ya ukaguzi, hufanywa na Maafisa wa Kazi
waliopo chini ya Kamishna wa Kazi.
   
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
     
         
 
Kazi [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158