JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
WATOTO
 
[ Jamii ] [ Jinsia ] Watoto [ Nyumbani ] au
 
 
    Mkoa umeendelea kusimamia na kutekeleza sheria na mikataba mbalimbali ya Kimataifa iliyoridhiwa na Serikali kuhusu haki na ustawi wa mtoto. Utekelezaji katika eneo hili unafanyika kwa ushirikiano na wadau mbalimbali.

Mafanikio :-
 • Elimu kuhusu haki na wajibu wa mtoto imetolewa katika shule za msingi 143 na Sekondari 52. Aidha, Watoto zaidi
  65,000 wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani ambayo hufanyika mwezi Juni ya kila mwaka.
 • Kila Halmashauri ya Manispaa imeunda baraza la watoto lenye wajumbe wasiozidi 60 kwa ajili ya kujadili masuala
  ya maendeleo.
 • Club za watoto zenye lengo la kuelimishana zimeundwa katika shuleni za msingi 124 na nyingine 41 katika
  mitaa ili kuwajenga watoto katika maadili mema na utunzaji wa mazingira.
 • Elimu ya athari za dawa za kulevya imetolewa kwa watoto na vijana 14,300 ukilinganisha na vijana/watoto 2,400
  kwa mwaka 2005. Aidha kipo kituo kimoja cha kurekebisha tabia kwa vijana walioathirika na utumiaji wa
  dawa za kulevya.
 • Hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya watoto 58 wa mitaani waliokuwa wanakitumika katika ukahaba, majumbani
  na mitaani.
 • Watoto 13,468 wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wasichana 6,050 na wavulana 7,418 wametambuliwa
  na wanapatiwa misaada ya kujikimu ikiwemo mahitaji ya shule, matibabu, matandiko, chakula, sabuni na viatu.
 • Kamati 158 zimeundwa ngazi ya mtaa ili kushughulikia matatizo ya watoto waishio katika mazingira hatarishi.
  Aidha kamati hizo zimepatiwa baiskeli 916 ili kurahisisha utendaji kazi. Pia mafunzo mbalimbali yametolewa kwa
  kamati zote 158 juu wajibu wa kamati na malezi ya watoto.
   
 
 
 
     
 
[ Jamii ] [ Jinsia ] Watoto [ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158