JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
 
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA
 
[ Nyumbani ]
 
 
[ MKUU WA WILAYA ] [ WABUNGE ] HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA [ KATA & MITAA ]
                           
Utangulizi
 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ipo kati ya Latitudo 6 na 7 kusini mwa Ikweta na kati ya Longitudo 39 na 40 Mashariki. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina eneo la kilomita za mraba 210 ambapo zaidi ya asilimia 75% ya eneo hilo la Manispaa ya Ilala ni eneo la mji.

Manispaa ya Ilala imepakana na Manispaa za Kinondoni na Temeke kwa upande wa Kaskazini na Kusini, Mkoa wa Pwani kwa upande wa Magharibi na Bahari ya Hindi katika ukanda wa Pwani wenye urefu Kilomita 10 kwa upande wa Mashariki.

 
 
 
Idadi ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya iliyofanyika Agost 2012, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya wakazi wapatao 1,220,611, ambapo idadi ya Wanaume ni 595,928 na na wanawake ni 624,683
 

 

Utawala
 
 
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imegawanyika katika Tarafa tatu (3) ambazo ni Ukonga , Ilala yenye , na Kariakoo yenye . ambapo ina jumla ya Kata Thelathini na tano (35) zikiwa na jumla ya Mitaa mia moja na hamsini na tatu (153)
Aidha Halmashauri ya Manispaa ina Majimbo matatu (3) ya Uchaguzi ambayo ni Ilala, Ukonga na Segerea.
Mstahiki Meya ni Kiongozi Mkuu na Mkurugenzi wa Manispaa ni Mtendaji Mkuu kwa upande wa Serikali za Mitaa. Manispaa inaongozwa na Baraza la Madiwani.

 

Shughuli kuu za Wakazi

Shughuli muhimu za kiuchumi katika Manispaa ya Ilala ni biashara, viwanda, kilimo na uvuvi pamoja na huduma za kiuchumi na kijamii. Pato la wastani la mkazi wa Manispaa ya Ilala ni sh.489, 204.00 kwa mwaka.

 

ELIMU YA AWALI

 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya shule/Vituo vya elimu ya awali 128 katika hivyo 76 ni vya serikali na 52 visivyo vya serikali.

 
 

ELIMU YA MSINGI

 

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ina jumla ya shule za msingi 158 kati yake shule 105 za serikali na 53 zisizo za serikali.

ELIMU YA SEKONDARI

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala inazo shule 91 za sekondari zikiwemo shule 49 za serikali na 42 zisizo za serikali. Aidha kuna vyuo vya ualimu 3 vinavyotoa Stashahada na Chet.i

 

 

ELIMU YA WATU WAZIMA NA ELIMU NJE YA MFUMO RASMI

 

Elimu ya Mfumo usio rasmi hutolewa kupitia Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa (MEMKWA), pia kwa watu wazima kupitia mpango wa uwiano kati ya elimu na jamii (MUKEJA) .

HUDUMA YA MAJI
Huduma ya maji katika Manispaa ya Ilala inategemewa kutoka kwenye vyanzo vikuu viwili ambavyo ni visima virefu na vifupi na maji ya bomba kutoka mto Ruvu. Idadi kubwa ya wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala hutegemea maji ya visima. Visima hivi vimechimbwa na Serikali, taasisi, mashirika na watu binafsi.

Halmashauri inashirikiana na wananchi katika uendeshaji wa miradi ya maji kwa njia ya Kamati za maji sambamba na kuimarisha mifuko ya maji ambayo imeanzishwa na wananchi.

AFYA
Huduma za afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, zinaendelea kutolewa kupitia jumla ya vituo vya tiba, Zahanati na hosptali za serikali, Mashirika ya dini na hiari (Non profit making Organisation) na taasisi binafsi.

 

 
Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
 
KILIMO NA MIFUGO
 

Halmashauri inalenga kutoa huduma za ugani kwa wakulima na wafugaji. Aidha inalenga kuthibiti magonjwa mbalimbali yanayoathiri mifugo na mazao yake kwa nia ya kuendesha kilimo chenya tija.

Halmashauri imeendelea kutoa huduma za ushauri kwa wafugaji na wakulima ambao hupatapatiwa mafunzo ya aina mbalimbali. Aidha, Wakulima na wafugaji hufanya ziara za mafunzo pia kuhudhuria maonyesho mbalimbali kama vile maonyesho ya viwanja vya Nanenane Morogoro.

Magonjwa ya mifugo yanaendelea kudhibitiwa kwa kuogesha na kutoa chanjo dhidi ya magonjwa mbali mbali ambapo Ng'ombe hupata chanjo ya chambavu na Kimeta, na chanjo ya Homa ya Mapafu.

Chanjo mbali mbali za Kuku kama vile chanjo ya Gumboro (IBD) na chanjo ya Mdondo hutolewa.

  


UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UBORESHAJI WA SERIKALI ZA MITAA
Halmashauri inatekeleza lengo la msingi la kujiimarisha ili iweze kutekeleza kwa ufanisi utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi wake hususani;

•  Utawala bora unaozingatia uwazi na Demokrasia

• Masuala ya Utumishi

Utawala wa sheria na ushirikishwaji wa umma hivyo kuinua ubora na kiwango cha utoaji wa huduma katika mazingira ya Utawala bora. Halmashauri imeendelea kufanya shughuli za maboresho katika maeneo ya Utawala bora, Utumishi, Fedha, Muundo na Sheria
 
 

BIASHARA NA SEKTA ISIYO RASMI:

 
 
Mpango mkakati wa Halmalshauri umelenga kuimarisha na kuboresha huduma za Biashara na Masoko, kutafuta maeneo ya kudumu kwa ajili ya biashara ndogo ndogo, kuongeza ajira na kuimarisha soko la ndani, kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa biashara pamoja na kuimarisha usimamizi wa sheria za biashara.
 
 
 
 
     
     
[ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213