JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
Siku ya Mtoto wa Africa yafana
 
Siku ya Mtoto wa Afrika [ Nyumbani ] au
 
 
Mkoa wa Dar es Salaam umeungana na watoto wengine wa Afrika katika Maadhimisho ya Siku ya ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Chimbuko la Siku ya Mtoto wa Afrika lilianza baada ya kupitishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa Kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini mwaka 1976.
Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Afrika imekuwa ikiadhimisha siku hii tangu mwaka 1991. Katika Bara zima la Afrika yanafanyika maadhimisho kama haya ambapo hapa Tanzania kwa mwaka huu 2015 yanaongozwa na Kaulimbiu, Tokomeza Mimba na Ndoa za Utotoni; Kwa Pamoja Tunaweza .

 

Wa kwanza kutoka kulia ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Edward Otieno

 
.

Maandamano ya watoto siku ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika

 

 
Watoto wakipita mbele ya Mgeni rasmi wakiwa na Bango lenye kauli mbiu maalumu ya siku ya Mtoto wa Afrika
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Siku ya Mtoto wa Afrika[ Nyumbani ] au
Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213