JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
BARABARA
 
[ Barabara ] Majengo [ Nyumbani ]
 
 
 
Utangulizi
 

Wakati wa uhuru (Desemba 9, 1961) Jiji la Dar es Salaam lilikuwa na barabara za lami zenye urefu wa km 155. Urefu huu unajumuisha barabara kuu pamoja na barabara za maeneo (area roads/streets) ambayo yalikuwa yameanza kuendelezwa kwa ajili ya makazi, maofisi pamoja na maeneo ya biashara. Maeneo haya ni Oysterbay, Kinondoni, Mwananyama, Magomeni (Quarters, Mapipa, Mikumi, Mwembe Chai), Ilala, Kariakoo, Temeke (Quarters) pamoja na Chang'ombe (wireless).

 

Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya barabara zenye urefu wa Km 3,262.74 ikiwa za lami ni km 736.9 , changarawe/ udongo ni km 2,525.84 Kati ya hizo km 600.97 ziko chini ya Wakala wa Barabara yaani TANROADS na km 2,661.77 ni za Halmashauri za Manispaa (Ilala km 804.37, Kinondoni km 811.1 na Temeke km 1046.3). Katika sekta hii mafanikio makubwa yamepatikana tangu mwaka 2005 hadi Disemba, 2013 kwani kulikuwa na jumla ya barabara zenye urefu wa km 444.21 zikiwa ni barabara za lami (Ilala km 79.85, Kinondoni km 178.8 na Temeke km 169.3) na km 1,009.36 za changarawe/ udongo. Kwa ujumla barabara za lami zimeongezeka kwa kiasi cha km 292.69 sawa na asilimia 39.7. Kwa upande wa madaraja mwaka 2005 kulikuwa na madaraja 28 hadi kufikia Disemba, 2013 kulikuwa na madaraja 133 ambayo ni ongezeko la Asilimia 79.

 

Barabara kuu (Trunk roads)

Barabara kuu ambazo ni barabara za Morogoro, Kilwa, New Bagamoyo Nyerere/Pugu, Mandela na Sam Nujoma zina urefu wa km 126.2 ambazo zinatumika kwa waingiao na watokao katika Jiji la Dar Es Salaam pamoja na barabara za Mkoa zenye urefu wa km. 368.3 zinasimamiwa na TANROADS. Barabara za Mkoa, Wilaya na barabara ndogo ndogo (feeder roads) zimeendelea kuongezeka kadri mji unavyoendelea kukua.

Aidha, kuna huduma nyingine za usafiri na usarishaji kama ifuatavyo:-
•  Reli za TRC na TAZARA inayotumika ndani ya Jiji na nje ya Jiji
•  Kiwanja kikubwa cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNIA)
•  Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni bandari kuu Pwani ya Afrika ya Mashariki kwenye Bahari ya Hindi

 

 

 

 

 
 
 
 
 
Ujenzi wa Daraja la Kigamboni eneo la Kurasini

 

Utekelezaji wa Mpango wa Matengenezo ya Barabara
Mkoa umeweza kufanya matengenezo maalum ya barabara mbalimbali kupitia TANROADS na Halmashauri za Jiji na Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke
 

Katika mwaka 2012/13, Serikali ilipanga kutekeleza miradi ya kujenga na kukarabati barabara za Jiji la Dar es Salaam ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Jiji ambapo utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali. Hadi Juni, 2013, kazi zilizofanyika ni kukamilisha ujenzi wa barabara za Ubungo Maziwa – External (km 2.25) na Ubungo Bus Terminal – Mabibo – Kigogo Round About (km 6.4); Jet Corner – Vituka – Davis Corner (km10.3) kwa asilimia 87 na Kigogo Round About – Bonde la Msimbazi – Twiga/Msimbazi Junction (km 2.7) kwa asilimia 72. Aidha, Serikali imekamilisha usanifu wa barabara na kuwapata wakandarasi wa ujenzi wa barabara za Tabata Dampo – Kigogo; Mbezi (Morogoro Road) – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km 14); Tegeta Kibaoni – Wazo Hill –Goba – Mbezi Mwisho (km 20); Tangi Bovu – Goba (km 9);Kimara Baruti – Msewe – Changanyikeni (km 2.6); Kimara –Kilungule – External Mandela Road (km 9) na Mwai Kibaki – Garden Road (km 9.1) . Vilevile ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo Haraka kutoka Kimara – Kivukoni, Fire – Kariakoo na Magomeni – Morocco umefikia asilimia 30. Kwa upande wa ujenzi wa Flyover ya TAZARA, utaratibu wa kumpata Mkandarasi unaendelea. Pia ujenzi wa mfereji wa maji kuanzia barabara ya Nyerere hadi Barabara ya Uhuru (Bungoni drain) umekamilika.

 

Kwa upande wa daraja la Kigamboni – Kurasini, daraja la muda limekamilika na kazi za ujenzi wa daraja imeanza ambapo nguzo 150 kati 202 zimekamilika na eneo la barabara zinazoingia katika daraja limesafishwa.

 

 

 
 
 
 
     
 
         
 
[ Barabara ] Majengo [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2860081/2863716, FAX: 022-2863716