JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
MIUNDOMBINU
 
Barabara [ Majengo ] [ Nyumbani ]
 
 
 
BARABARA
 

Mtandao wa barabara za Mkoa wa Dar es Salaam una urefu wa km 2094.4 ambapo kati ya hizo TANROADS inasimamia na kuhudumia barabara zenye urefu wa km 494.3 na zilizobaki km 1600.1 ziko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4). Halmashauri ya Jiji haina barabara inayoisimamia.

 
 
 
Mtandao wa barabara umegawanyika katika makundi yafuatayo:
•  Barabara kuu (Trunk roads):
Barabara kuu zote ambazo ni barabara za Morogoro, Kilwa, New Bagamoyo, Nyerere/Pugu,na Mandela/Sam Nujoma zina urefu wa km 126.2

 

•  Barabara za Mkoa (Regional Roads):
Barabara za Mkoa zote zinazosimamiwa na TANROADS zina urefu wa km 368.3

 
 

Barabara zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa

•  Barabara za Halmashauri (District & Feeder roads)
Barabara za Halmashauri ni zile zenye urefu km 1600.1 zilizoko chini ya usimamizi wa Halmashauri za Manispaa za Ilala (km 429), Kinondoni (km 692.7) na Temeke (km 478.4).

 

 

 

 

Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara Mkoani

 
Kwa kushirikiana na Shirika la Msaada la JAPAN (JICA) mpango kabambe wa usafiri na usafirishaji umeandaliwa. Mpango huu utatumika katika uendelezaji wa ujenzi wa miundo mbinu na aina mbalimbali za usafiri na uchukuzi hadi mwaka 2030.
 

 

 

 
 
 
 
 
 

Jedwali la Mtandao na Aina za Barabara Mkoani
Dar esSalaam

 

Msimamizi

Urefu wa Barabara(km) Aina ya barabara(km)
Lami Changarawe Udongo
Tanroads
494.3
211.4
282.9
Ilala
429
132
80
217
Kinondoni
692.7
114.7
315.25
262.752
Temeke
478.4
67
411.11
Jumla
2094.4
525.1
1569.3

 

 

 
 
.

 

 
 
 
     
     
 
 
Barabara [ Majengo ] [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, P.O.Box 5429, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213