JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
UPIMAJI
 
[ Ardhi ] Upimaji [ Rudi nyumbani ]
 
 
    Upimaji Ardhi Na Ramani
   

 

   

Kati ya miaka 1999 -2006, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilichukua mikakati ya kupima viwanja katika mradi ya viwanja Elfu Ishirini. Viwanja zaidi ya 45,000 vilipimwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji. Mradi huu kwa sasa umehamishiwa kwenye Halmashauri za Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke kuanzia mwaka 2008.

Halmashauri zimekuwa na jitihada mbalimbali za kupima viwanja lakini kutokana na uwezo mdogo wa kifedha imewawia vigumu hususan katika utwaaji wa maeneo kwa ajili ya upimaji viwanja. Mathalani, Halmashauri za Manispaa zilikopeshwa fedha na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya Mradi na upimaji viwanja na kuboresha makazi.

Mwaka 2005 vimepimwa viwanja 2,740 hadi kufikia Disemba, 2013 kuna viwanja 36,289 kufanya ongezeko la jumla ya viwania 33,549 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Taratibu za Kuomba Upimaji Ardhi:

Taratibu za kuomba upimaji ardhi huzingatia sheria ya upimaji kwa kuzingatia utaratibu ufuatao:

i. Mwombaji wa upimaji ardhi huandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya husika akiambatanisha na nyaraka za ununuzi wa eneo hilo au nyaraka za kuthibitisha eneo hilo ni lake, Barua hiyo vile vile aipitishwe kwa Mwenyekiti wa Mtaa husika na kisha kwa Afisa Mtendaji wa Kata ambako eneo lake lilipo.

ii. Baada ya barua hiyo kupokelewa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika, Mkurugenzi huwasilisha barua hiyo katika Idara ambayo inahusika na sekta ya Ardhi ndipo Afisa Ardhi Mteule anathibitisha uhalali wa umiliki ardhi hiyo inayoombewa upimaji.

iii. Afisa Ardhi atajazo fomu SF.47 kwenda kwa Afisa Mipangomiji ili kuthibitisha iwapo eneo ambalo liliombewa upimaji ardhi kunamchoro wa mipangomiji ambao unaendana na mipaka na maombi ya matumizi ya ardhi ya mhusika.

iv. Afisa Mipangomiji akithibitisha mchoro unaendana maombi atawasilisha fomu SF.47 kwa Afisa Ardhi Mteule.

v. Afisa Ardhi akipokea fomu hiyo SF.47 ndipo anawasilisha maombi ya upimaji wa eneo hilo kwa kujaza fomu SF.37 akiambatanisha na Mchoro wa mipangomiji wa eneo husika.

vi. Mpima Ardhi atatoa maelekezo ya upimaji ardhi kwa mpima atayefanya upimaji wa eneo hilo kwa kuzingatia sheria na kanuni za upimaji ardhi

   
     
     
     
     
     
     
     
     
     
     
   
   
   
   
   
     
         
 
[ Ardhi ] Upimaji [ Ramani ] [ Rudi nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203158