JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
 
     
ARDHI
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Nyumbani ]
 
 
 
Utangulizi
 

Umiliki wa Ardhi

 

Baada ya miaka 52 ya Uhuru maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam yalikaliwa na wazawa ambapo maeneo hayo yapo kati ya eneo la kati la biashara (CBD) Kariakoo, Ilala, Magomeni yamekuwa yakiuzwa kwa watu wenye uwezo wa maendelezo ya majengo ya ghorofa.

Utoaji wa miliki za Ardhi umekuwa ukitolewa kwa kasi na kwa kutumia TEKNOHAMA ikilinganishwa na miaka kabla ya Uhuru hadi miaka ya 1999.

Baada ya Halmashauri ya Jiji kuvunjwa na Tume ya Jiji kuwepo na kisha baadaye Halmashauri tatu za Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke kuundwa mwaka 2000 idadi ya Hati miliki nyingi zimetolewa.

Hata miliki za viwanja zimekuwa zikitolewa kwa ushirikiano na Wizara ya Ardhi ambayo imeunganishwa na Halmashauri kwa njia ya Mtandao. Vile vile, kodi za Ardhi zimekuwa zikikusanywa kwa utaratibu huo.

Baada ya miaka 52 ya Uhuru sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 namba 4 na 5 Ardhi imekuwa ikitumika na thamani katika miaka 52 ya Uhuru ni wazi kuwa thamani ya utwaaji Ardhi imekuwa ni ghali ikilinganishwa na wakati kabla ya Uhuru.

Uendelezaji upya wa eneo la magomeni Quarter

 

Uzoefu wa Miaka 52 ya Uhuru ni kuwa viwanja vimeanza kuuzwa kutokana na upandaji wa gharama za utwaaji, upimaji na uandaaji miliki ya viwanja baada ya sheria namba 4 ya Ardhi ya mwaka 1999 kuanza kutekelezwa. Uuzaji viwanja ulianza rasmi kwenye Mradi wa Upimaji viwanja elfu ishirini (20,000) chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Maeneo ya Viwanja vya masafa ya chini (Low Density Plot) yalijulikana kama Uzunguni, masafa ya kati yakiwa Uhindini na masafa ya juu (High Density) kwa wananchi wa kawaida. Miliki ya viwanja vya masafa ya chini Low Density ni miaka 99, kwa viwanja vya masafa ya kati miaka 66 na miaka kwa viwanja vya masafa ya juu kuwa miaka 33. Offer au Hati za muda zilitolewa na baadaye hati za kudumu.

Mwaka 2005 zilitolewa Hati miliki 7,125 Wakati 2013 zilitolewa 19,111 , kwa ujumla katika kipindi hiki hadi Disemba, 2013 zimetolewa jumla ya hati miliki 26,236 Aidha, mwaka 2005 leseni za makazi zilianza kutolewa hadi Disemba, 2013 zimetolewa jumla ya leseni za makazi 51,049 katika Mkoa wa Dar es Salaam.

 

 
 
 

 

 
 
 

 

 

Mapendekezo ua Uendelezaji wa wa eneo la Mchikichini

 

Mipangomiji na Udhibiti wa Matumizi Bora ya Ardhi.

Mamlaka ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mpango wa matumizi ya Ardhi hata kabla ya Uhuru ambapo maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali yalitengwa. Matumizi hayo kulingana na mpango kabambe yalitengwa kwa kuzingatia matabaka ya watu na uwezo wa kifedha.

Aidha, kuongezeka kwa uhitaji wa viwanja na kupungua kwa uwezo wa Mamlaka za Jiji kupewa viwanja vilivyopimwa yalisababisha makazi holela kuongezeka.

Baada ya miaka 52 ya Uhuru Mamlaka za Halmashauri za Manispaa za Jiji la Dar es Salaam zimekuwa na mikakati mbalimbali ya kuandaa matumizi ya Ardhi, kuendeleza upya maeneo ya kati, kudhibiti ukuaji holela wa makazi, kurasimisha makazi holela na kuandaa mpango kabambe wa Jiji. Mpango wa uendelezaji upya na maeneo ya Kariakoo, Upanga, Msasani, Temeke, Ilala, Magomeni, Msasani na Osterbay umeandaliwa na kuanza kutekelezwa.

Ukuaji wa Jiji umefanyika kwa kila upande ukielekea kwenye njia kuu za kuingia katikati ya Jiji kwenye Bandari. Ukuaji huo zaidi ya asilimia 75 ni makazi holela na asilimia 25 ni maeneo yaliyopangwa kimipangomiji na kupimwa. Aidha Serikali imekuwa na juhudi mbalimbali za kudhibiti uendelezaji holela wa Jijini kama vile uanzishaji wa Mamlaka za Uendelezaji Mji wa Kigamboni inayoitwa Kigamboni Development Agency (KDA). Mamlaka hii imepewa mamlaka ya kusimamia na kuratibu uendelezaji upya wa eneo la Kigamboni kuwa Jiji la Kisasa na lenye hadhi ya Kimataifa.

Kulingana na mpango kabambe wa Jiji la Dar es Salaam ulioko kwenye hatua za maandalizi, Mkoa wa Dar es Salaam una ardhi yenye eneo la hekari 161,796,384 ambazo ni sawa na kilometa za mraba 1,617.96.

 

 

 
 

 

 
 

 

 
 

 

 
 

 

 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
     
 
 
Ardhi [ Upimaji ] [ Ramani ] [ Nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213