JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA - OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA      
 
     
   
     
AFYA
 
Afya [ Rudi nyumbani ]
 
 
 
Utangulizi
 

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Mkoa wa Dar es Salaam una idadi ya watu takribani 4,369,541 sawa na ongezeko la asilimia 5.6 kwa mwaka, kutokana na ongezeko la kawaida pamoja na wahamiaji wa ndani ya nchi wanaokuja kibiashara na kutafuta maisha mazuri; ambao wanaishi kwenye mitaa ipatayo 452. Idadi hii ya watu inapata huduma za afya kinga na tiba kupitia vituo vya kutolea huduma vya Serikali, Mashirika ya dini na yasiyo ya Kiserikali na Sekta binafsi.

 
 
 

Sekta ya Afya katika ngazi ya Mkoa inaongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa akisaidiwa na Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya Mkoa (RHMT).

 

 

hadi kufikia mwaka 2013 Mkoa wa Dar es salaam una jumla ya idadi ya zahanati 392 kati ya hizo Zahanati za Serikali ni 89 na za mashirika/watu binafsi ni 303

Kuna jumla ya Vituo vya Afya 24 kati ya hivyo vituo vya serikali ni 5 na mashirika / watu binafsi ni 27. Hata hivyo, Vituo vya Afya 3 vimeshapandishwa hadhi na kuwa Hospitali (Mnazi Mmoja, Mbagala Rangi Tatu na Sinza)

Aidha,kuna jumla ya Hospitali 36 kati ya hizo 7 ni za Serikali na za watu binafsi ni 29.

Kwa ujumla huduma za afya zimeimarika, idadi ya magari ya kubebea wagonjwa (ambulance) ni 19. Ujenzi wa Zahanati unaendelea kwenye maeneo yaliyo pembezoni katika kila Halmashauri zote.

 
 
 

 

 

 

 
 
 
 

Hospitali za Amana, Mwananyamala na Temeke zimepandishwa hadhi kuwa za Rufaa za Mkoa na hivyo kuziwezesha kuwa na Madaktari Bingwa wa magonjwa ya ndani (Internal Medicine) upasuaji, mifupa, watoto na uzazi wapatao kufikia 27. Hii, imesaidia kupunguza rufaa zisizo za lazima kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, Hospitali ya Amana inatoa huduma ya kupima magonjwa ya mfumo wa chakula kwa kutumia kipimo kijulikanacho kama endoscope ambapo awali kilikuwa kikipatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa kutambua mchango wa maambukizi ya VVU katika vifo vinavyotokana na uzazi, Mkoa umezindua mpango wa kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto unaojulikana kama 'option B+' ambao pia unampa mama fursa ya kuanza dawa ya kupunguza makali ya VVU mara tu anapogundulika kuwa na maambukizi ili kuimarisha kinga ya mwili hivyo kuboresha afya na maisha yake kwa ujumla.  

 

Pamoja na jitihada zinazofanyika bado Mkoa unakabiliwa na upungufu wa vituo vya kutolewa huduma za Afya na watumishi ukilinganisha na idadi kubwa ya watu wanaohitaji huduma hiyo kufuatia kasi kubwa ya watu wanaoingia Mkoa wa Dar es Salaam. Mkoa umechukua hatua mbalimbali ikiwemo, kujenga hospitali na vituo vipya vya tiba, kukarabati na kupanua majengo ya kutolea huduma pamoja na kuboresha vyanzo vya mapato ikiwemo kuhamasisha wanachi kujiunga na mpango wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Mkoa unaendelea kuajiri watumishi wenye sifa na ujuzi mbalimbali ili kupunguza tatizo la upungufu wa watumishi.

 
 
     
     
 
         
 
Afya [ Rudi nyumbani ]   Rudi juu
 
     
Copyright © 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, TEL: 022 - 2203156/2203158, FAX: 022-2203213